Mgomo mkubwa wa wafanyakazi unafanyika Afrika kusini
Mgomo mkubwa wa wafanyakazi unafanyika
Wafanyakazi wamemiminika katika miji mikubwa Afrika kusini
Muungano mkubwa wa vyama vya wafanyakazi Afrika kusini - Cosatu - unafanya mgomo wa kitaifa kupinga rushwa.
Kunatarajiwa kuwa na migomo 13 katika miji yote mikuu ikiwemo miji mikubwa kibiashara Johannesburg, Cape Town na Durban.
Makundi ya wafanyakazi tayari wameanza kukusanyika.
Katibu mkuu wa muungano wa Cosatu, Jumatano aliwaambia waandishi habari kwamba maandamano hayo yatakuwa makubwa kushinda maandamano mengine yote.
"Tunatumia mgomo kutuma ujumbe kwa serikali na sekta ya kibinfasi kwamba tumechoka na rushwa katika jamii yetu," ameeleza.
Hatua hiyo inaungwa mkono na mshirika mwingine wa chama tawala ANC, chama cha SACP.
Inaarifiwa pia kwamba waandamanaji watashinikiza kujiuzulu kwa rais Zuma.
Cosatu imekuwa ikimuunga mkono rais Zuma lakini sasa unamuunga mkono naibu rais Cyril Ramaphosa katika kuwania uongozi dhidi ya Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Afrika anayeonekana kupendelewa na rais Zuma kumrithi
Comments
Post a Comment