SERIKALI Yaendelea Kumkaba Koo Freeman Mbowe....
Serikali imetoa siku 30 kwa wawekezaji 50 waliopewa maeneo ya kujenga viwanda na kushindwa kuvijenga, kuwasilisha mipango ya ujenzi vinginevyo watanyang’anywa. Serikali imetoa orodha ya watu hao na taasisi zilizopewa maeneo katika eneo la Weruweru karibu na kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools, akiwamo mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe. Katika orodha hiyo, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Taifa wa Chadema anaonekana kumiliki viwanja viwili; kimoja kikiwa na ukubwa wa hekta 1.88 na kingine na hekta 2.17. Akizungumzia uamuzi huo mpya wa Serikali na sababu za kushindwa kuendeleza eneo hilo kwa miaka 13 tangu yeye na wenzake walipomilikishwa mwaka 2004, Mbowe alisema alikuwa hajapata taarifa hizo, lakini kwa vile yuko njiani kuelekea mkoani Kilimanjaro akifika atafuatilia. Ataja sababu Mwanasiasa huyo alisema Serikali inapaswa kulaumiwa kwa kutofikisha miundombinu muhimu katika eneo hilo ikiwamo umeme na badala kutarajia wawekezaji wabebe gharama hizo. Aliongeza kuwa ni vigumu waw...