ALIYEKUWA Miss Kinondoni, Diana Edward ndiye mlimbwende wa Tanzania 2016 baada ya kuwashinda wenzake 29 katika viwanja vya Rock City Mall juzi usiku mkoani hapa. Mashindano hayo makubwa kabisa hapa nchini yaliamuliwa na majaji ambao ni Rita Mbelo,Catherine Kibaso,Sophia Masei,Raphael Siantini,Joe Makanyaga,Eliza Kilili,Juma Sultan,Prashant Patel na Ramesh Shah. Mashindano hayo yalianza kwa warembo kucheza nyimbo mbali mbali kabla ya kutinga na mavazi ya ubunifu,ufukweni na vazi la jioni. Jaji Shah aliweza kuwataja warembo walioingia 15 bora ambao ni Anna Nitwa,Sia Pius,Lisa Ndolo,Grace Malikita,Eunice Robert,Regina Ndimbo,Iluminata Dominic,Sporah Lulende na Maria Peter. Wengine ni Maureen Ayoub,Queen Nazir,Julietha Kabete,Maureen Kamanya na Abel John. Patel aliwataja warembo walioingia 5 bora ambao ni Grace Malikita,Anna Nitwa,Maria Peter,Julietha Kabete na Diana Edward. Jaji Prashant Patel aliweza kutangaza warembo walioingia tatu bora, ambao ni Diana Edward aliyeibuka ms...