Posts

Showing posts from September 18, 2016

AliKiba na Diamond Kuoneshana jeuri ya Pesa

Image
Mziki wa bongo fleva umepata umaarufu mkubwa sana Barani Afrika na Duniani kwa ujumla. Kitendo hiki cha mziki wetu kuvuka border kimesaidia sana kuongeza Ajira kwa vijana na kukuza vipato vya wasanii wetu. Miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri ni Alikiba na Diamond. Wasanii hawa wawili wamejikita zaidi kuutangaza mziki wetu kimataifa hivyo kujipatia umaarufu mkubwa sana. Na kama tunavyojua Umaarufu ni moja kati ya vitu vitakavyokufanya upate pesa kwa uraisi zaidi. Msanii Diamond platnumz amejikita zaidi kuwekeza katika Ardhi kama anavyosema mwenyewe "Najenga vibanda" na mpaka sasa ana vibanda zaidi ya viwili vimesimama kama "Kangaroo" Kwa upande wa kiba bado sijajua anamiliki Vibanda vingapi ila najua ancho hata kama ni kimoja ila tu hapendi kujionesha. Hivi majuzi tulipata tetesi ya kuwa anataka kununua gari yenye thamani ya M700 na pia anataka kununua Helikopta kwaajili ya kumfikisha hapa na pale huku Hasimu wake nae inasemekana anataka kununua Bot...

Gavana wa Benki Kuu (BoT) Benno Ndulu, na Msajili wa Hazina Kizimbani Leo

Image
Mahakama  Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemtaka Gavana wa Benki Kuu (BoT) Benno Ndulu, na Mwendeshaji wa benki ya FBME, Lawrence Mafuru, wafike mahakamani kujieleza jinsi watakavyotekeleza amri iliyoitaka BoT kulipa Sh bilioni 92. Maofisa hao wanatakiwa kuieleza mahakama watakavyoilipa kampuni ya Coast Textiles Ltd fedha hizo na kama watashindwa kufanya hivyo, watafungwa jela kama wafungwa wa kesi ya madai. Utekelezaji wa amri hiyo unatokana na uamuzi wa shauri namba 129 la mwaka 2009, ulioiamuru benki ya FBME kuilipa kampuni ya Coast Textiles Ltd fedha hizo baada ya kukamata kiwanda chake na kukiuza kwa kampuni ya Five Star Investment ltd. Uuzwaji wa kiwanda hicho ulitokana na mgogoro wa ulipaji mkopo ambao kampuni ya Coast iliuchukua katika benki hiyo. BoT inahusishwa kwenye shauri hilo kutokana na kuchukua uendeshaji wa benki ya FBME baada ya benki hiyo kuhusishwa na utakatishaji fedha nchini Cyprus. Maofisa hao walitakiwa kufika mahakamani hapo Septemba 16 mwaka h...

M-Pawa yazidi Kuwatajirisha Watanzania Mshindi wa Pili wa Milioni 20 Apatikana

Image
Vodacom Tanzania wakishirikiana na Benki ya CBA, ilizindua promosheni kubwa inayojulikana kama “Jiongeze na M-Pawa” ambayo inawawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pawa kujishindia zawadi ya fedha taslimu. Meneja masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati) akiongea na mmoja wa mshindi wa droo ya promosheni ya Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za M-Pawa wa Benki ya CBA Eric Luyangi na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100. Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja. Promosheni hiyo ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi wa 9 i...

TBC yaendesha Harambee ya kuchangia waathirika wa tetemeko la Ardhi KAGERA

Image
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, NAPE NNAUYE ameanza kupokea msaada kupitia harambee Mwenyekiti wa Kampuni ya Skol Building Contractors Limited Bw.Vincent Massawe (kushoto) akikabidhi Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. NAPE NNAUYE Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo, NAPE NNAUYE ameanza kupokea msaada kupitia harambee iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kwa ajili ya waathirika tetemeko la ardhi lilitotokea mkoani KAGERA mapema mwezi huu.          Akipokea mchango wa shilingi milioni 10 uliotolewa na kampuni ya  ujenzi  ya SKOLL BUILDING CONSTRUCTORS LTD jijini DAR ES SALAAM, Waziri NNAUYE amewataka wadau wengine kujitokeza kuwasaidia waathirika hao. Kwa upande wake Mwenyekiti wa BUILDING CONSTRUCTORS LTD VINCENT PETER amewaomba wafanyabiashara kutoa michango yao ILI kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo.

Serikali yawaondolea vikwazo wawekezaji

Image
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. JULIANA PALLANGYO amesema serikali imeondoa vikwazo kwa wawekezaji nchini Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. JULIANA PALLANGYO Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. JULIANA PALLANGYO amesema serikali imeondoa vikwazo kwa wawekezaji nchini na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara ili kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini. Akizungumza mara baada ya kufungua semina ya makubaliano ya Biashara ya Nishati kati ya TANZANIA na NORWAY Dkt PALLANGYO amesema serikali imeunda sera za kitaifa na sheria mbalimbali ili kuwawezesha wawekezaji hao kufanya biashara kwa kufuata sheria za nchi. Naye Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara Prof. JOSEPH MKENDA amesema mkutano huo utajadili namna wawekezaji kutoka NORWAY wanaweza kuwekeza nchini TANZANIA husuani katika sekta ya nishati.

Ajali ya basi la SUPERSHEM yaua 11 mkoani MWANZA

Image
Watu 11 wanahofiwa kufa katika ajali iliyohusisha basi la SUPERSHEM na daladala katika barabara kuu ya MWANZA – SHINYANGA Watu 11 wanahofiwa kufa katika ajali iliyohusisha basi la SUPERSHEM na daladala katika barabara kuu ya MWANZA – SHINYANGA. Akizungumza na TBC kwa njia ya simu Mkuu wa mkoa wa MWANZA, JOHN MONGELLA amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitatolewa baadae. Amesema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa MWANZA inaelekea katika eneo la ajali wilayani KWIMBA. Taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo tutawaletea katika taarifa zetu za habari zijazo.

Mwenyekiti wa NCCR MAGEZI ahimiza watanzania kujenga Amani

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha NSSR-Mageuzi JAMES MBATIA amesema njia pekee kwa watanzania ya kujenga amani Mwenyekiti wa Chama Cha NSSR-Mageuzi JAMES MBATIA Mwenyekiti wa Chama Cha NSSR-Mageuzi JAMES MBATIA amesema njia pekee kwa watanzania ya kujenga amani ni kufanya kazi kwa bidii na kutenda haki katika maisha yao ya kila siku. Katika mahojiano maalum na TBC jijini DSM kuhusu siku ya amani duniani MBATIA amesema ni muhimu kwa watanzania wakajijengea mioyo yao kuwa ya upendo na mshikamano ili kulinda amani iliyopo. Naye Mhadhiri wa chuo cha Diplomasia, ISRAEL SOSTENES   amesema baadhi ya mila na desturi zinazochangia kutokea kwa migogoro katika bara la AFRIKAna kusababisha kukosekana kwa amani. SOSTENES amesema mgawanyiko huo ulisababishwa  na historia ya ukoloni pia umezifanya nchi za AFRIKA zikose  misingi ya utawala bora wa kidemokrasia licha ya nchi hizo kupata uhuru. Aidha SOSTHENES amesema tabia ya ubinafsi ya baadhi ya viongozi wa bar...

Wamarekani waandamana kupinga mauaji ya mtu mweusu

Image
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Maandamano Marekani Maandamano yamezuka kwa siku wa pili mfululizo katika mji wa Charlotte, Marekani, kufuatia kifo cha mtu mmoja mweusi aliyepigwa risasi na polisi, Jumanne usiku. Polisi wa kuzuia ghasia wametumia mabomu ya machozi kutawanya umati mkubwa wa watu wenye hasira waliokuwa wamekusanyika katikati ya mji. Katika ghasia hizo mtu mmoja aliuawa kwa risasi. Serikali katika eneo hilo imeyaita mauaji hayo kama ya raia kwa raia. Maandamano na Ghasia zilizuka Jumanne usiku baada ya polisi kumuua Keith Lamont Scott, huku wakisema kwamba kijana huyo alikuwa na bunduki na kwamba alipuuza wito wa kuweka silaha chini. Hata hivyo familia ya kijana huyo imesema kuwa hakuwa amebeba silaha yoyote Meya wa mji huo, Jennifer Roberts, ameiambia BBC kuwa aliwataka polisi kumwonyesha mkanda wa video ya tukio hilo.

Simba yaishtukia Yanga mapema, yamficha Ajib

Image
NA HUSSEIN OMAR SIMBA imeshtuka mapema kabisa naimeamua kumficha straika wake tegemeo, Ibrahim Ajib, ili kumwepusha na kadi nyingine ya njano ambayo inaweza kumsababisha akakosa pambano la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga litakalochezwa Oktoba 1, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Ishu kamili iko hivi:-Ajib ana kadi mbili za njano iwapo akipata kadi nyingine ya tatu kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Majimaji,basi atalazimika kukaa nje kwenye pambano la Oktoba 1, dhidi ya Yanga kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi moja ambayo itaambatana na kadi hiyo. Katika kuhakikisha hilo halitokei, inaonekana Simba wameamua kumweka benchi kwenye mechi dhidi ya Majimaji ili asiwe hatarini kulikosa pambano la kisasi dhidi ya Yanga mwanzoni mwa mwezi ujao. Hilo limethibitika kwenye mazoezi ya timu hiyo jana jioni katika Uwanja wa Boko Veteran nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kocha wa Simba, Joseph Omog, kuonekana kumwandaa Ame Ali kuziba nafas...

Waasi wasema watu 100, wauawa DRC, wakati wa maandamano

Image
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Rais Joseph Kabila wa DRC Waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kiasi cha watu mia moja wameuawa katika maandamano ya kuipinga serikali, katika kipindi cha siku tatu zilizopita. Vyanzo vingine vya habari vinasema watu waliouawa ni 40. Ofisi ya Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila imepinga taarifa hizo, huku ikiwalaaumu viongozi wa maandamano hayo kwa kuchochea ghasia hizo za umwagaji damu. Upinzani nchini humo wamevilaumu vyombo vya usalama kwa kuwashambulia kwa risasi watu waliokuwa wakiandamana kwa amani juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Rais nchini humo. Wanaamini kuwa Rais Kabila anajaribu kung'ang'ania madaraka hata baada ya kumalizika kwa muhula wake.

Marekani na Urusi zatupiana maneno juu ya Syria

Image
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Moja ya malori yaliyoteketezwa Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano. Wamarekani wamekuwa wakiamini kuwa Urusi ndio iliyoshambulia msafara huo, huku Warusi wakilipinga hilo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi John Kerry, alitoka nje ya lugha ya kidiplomasia kwa kutumia dhihaka zaidi. Huku mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov akipinga hisia hizo kali kwa kuorodhesha mifano kadhaa kutetea nchi yake. Aidha ametaka pia kufanyika Licha ya majibizano makali, Urusi na Marekani zilikubaliana kwa pamoja kuongoza mkutano wa mataifa 23, yanayoiunga mkono Syria ambao utafanyika mjini New York, baadaye leo. Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umesema unajiandaa kuanza tena kutoa misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria, baada ya kusitishwa kwa usambazaji wa mis...

Watumishi wa umma wachangisha zaidi ya Bil 1 kusaidia waathirika wa tetemeko

Image
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi JOHN KIJAZI amewasilisha kwa Waziri Mkuu hundi ya zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni michango ya watumishi wa umma Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA, akikabidhiwa mfano wa hundi na Katibu Mkuu Kiongozi aliyeongozana na Msajili wa Hazina LAWRENCE MAFURU Katibu Mkuu Kiongozi Balozi JOHN KIJAZI amewasilisha kwa Waziri Mkuu hundi ya zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni michango ya watumishi wa umma kutoka katika wizara, idara na taasisi zote za umma nchini kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi la Septemba 10 mkoani KAGERA. Akikabidhi hundi hiyo kwa Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA, Katibu Mkuu Kiongozi aliyeongozana na Msajili wa Hazina LAWRENCE MAFURU amesema wafanyakazi wameguswa na janga hilo na hivyo kuwasaidia wananchi hao ili kukabaliana na changamoto iliyowapata. Katibu Mkuu Kiongozi amesema michango mingine inaendelea kuchangwa ambapo ikikamilika itakabidhiwa kwa Waziri Mkuu kwa malengo ya kusaidia waliokumbwa na janga hilo....

Rais MAGUFULI amtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE

Image
Rais Dkt. JOHN MAGUFULI ametumia salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la Kampuni ya New Force Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI  Rais Dkt. JOHN MAGUFULI ametumia salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la Kampuni ya New Force iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika Kijiji cha LILOMBWI, Kata ya KIFANYA, tarafa ya IGOMINYI Mkoani NJOMBE.         Basi hilo lililokuwa linatokea jijini DSM kwenda SONGEA  mkoani RUVUMA lilipinduka na kuuwa watu 12 na wengine 28 kujeruhiwa. Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema  katika salamu hizo kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. REHEMA NCHIMBI, Rais MAGUFULI amesema amepokea taarifa za ajali hiyo kwa masikitiko na kwamba anaungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliopatwa na msiba katika kipindi kigumu cha majonzi.         ...

ALICE KELLA - SIRI SIRI VIDEO

Image

EFL: Chelsea watoka nyuma na kulaza Leicester City

Image
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Ilikuwa mara ya kwanza Cesc Fabregas kufunga msimu huu Cesc Fabregas alifunga mabao mawili muda wa ziada na kusaidia Chelsea kujikwamua na kulaza Leicester City katika mechi ya raundi ya tatu Kombe la Ligi (EFL). Leicester walikuwa wamesalia wachezaji 10 wakati wa kumalizika kwa mechi baada ya Marcin Wasilewski kupewa kadi nyekundu dakika ya 89. Muda mfupi kabla ya mapumziko, Chelsea walikuwa 2-0 nyuma kutokana na mabao ya Shinji Okazaki dakika ya 17 na 34 lakini Gary Cahill alikomboa moja muda mfupi kabla ya kipenga cha mapumziko kupulizwa. Cesar Azpilicueta alisawazisha kwa kombora la mbali dakika ya 49. Fabregas, 29, aliwaweka mbele kwa bao alilofunga dakika ya 92 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 94. Wasilewski alioneshwa kadi ya pili ya njano kwa kumgonga kwa kiwiko cha mkono mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa. Image copyright REUTERS Image caption Kurejea kwa David Luiz hakujawasaidia Chelsea kuziba mianya safu ya ulinzi I...

Picha: Ndege ya kwanza ya ATCL yatua Dar

Image
Hatimaye mwali amewasili. Ni ndege ya kwanza ya ATCL, Bombadier Q400 NextGen. Bombadier Q400 NextGen baada ya kuwasilia JNIA, Dar Jumanne hii Ndege hiyo imetokea Canada ilikotengenezwa na kupokelewa kwa shangwe huku mapokezi hayo yakiongozwa na katibu mkuu wa uchukuzi, Dkt Leonard Chamriho Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 76 ambao ni tofauti  na wahudumu na Rubani Ndege ya pili itawasili baada ya wiki moja na Rais John Magufuli ataongoza mapokezi rasmi ya ndege hizo

Maroune Fellain: Wachezaji Manchester United tunatakiwa kuwajibika

Image
Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Maroune Fellain amekiri kuwa wapo katika wakati mgumu baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo Fellain amefunguka kuwa yeye na wachezaji wenzake wanatakiwa kuwajibika katika hali chanya wakianza na mchezo wa kesho jumatano wa EFL Cup dhidi ya Northampton. Wakati akiongea na kituo cha TV cha France SFR Sport Fellain amesema. “Tunaweza kusema ni anguko dogo kwa sababu klabu Man United haiwezi kupoteza mechi 3 ” “Ndiyo ni dogo , lakini sisi ni wanaume na lazima tusimame pamoja na kuonesha”

Guardiola: Yaya Toure lazima aombe msamaha la sivyo hatocheza tena

Image
Kochaa wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amefunguka kuwa hatomchezesha tena Yaya Toure hadi atakapoomba msamaha kwa klabu hiyo na wachezaji wenzake kutokana na matamshi ya ajenti wake. Toure mwenye umri wa miaka 33 ameichezea City mara moja msimu huu na aliwachwa nje katika kikosi cha vilabu bingwa Ulaya. Ajenti wake Dimitri Seluk amesema kuwa kiungo huyo wa kati ”alifedheheshwa” na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City haitashinda kinyang’anyiro hicho. Guardiola:”lazima aombe msamaha la sivyo hatocheza”. Raia huyo wa Uhispania pia anataka msamaha kutoka kwa Seluk. Alisema kuwa ni uamuzi mgumu kumwacha nje Toure katika kikosi cha kombe la Vilabu bingwa Ulaya. ”Iwapo ana tatizo anafaa kuzungumza wenzake katika klabu ,alisema Gurdiola,ambaye alikuwa mkufunzi wa Barcelona wakati Toure alipouzwa kwa Manchester City 2010.

Marekani yaitupia lawama Urusi, shambulio la Syria

Image
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Madhara ya vita Syria Marekani imesema ndege za kivita za Urusi zilihusika kushambulia msafara wa misaada nchini Syria siku ya Jumatatu na kusababisha vifo. Maafisa wa Marekani wameiambia BBC ndege mbili za kivita za Urusi aina ya SU-24, zilikuwa angani, sambamba na msafara huo wa magari, wakati tukio hilo likitokea. Hata hivyo Urusi imekana na kusema kuwa ndege hizo hazikuwa zake wala za Syria, na kutupia lawama wapiganaji wa waasi. UN wasitisha usafirishaji misaada Syria Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege zake zinazojiendesha zenyewe zilikuwa zikifuatilia msafara huo, lakini kamera zao zilijizima kabla ya mashambulizi kuanza. Shambulio hilo la Jumatatu lilifanyika saa kadhaa baada ya serikali ya Syria kutangaza kumaliza wiki ya kusitisha mapigano

Wema: Nilitaka mil 75 kuwa Salome, WCB wakanipa mil 50 nikakataa

Image
Mwanadada Wema akiongea na kipindi kimoja cha redio leo mchana alipoulizwa yapi maoni yake kuhusu wimbo mpya wa Salome alisema wimbo ni mzuri sana na alitakiwa kufanya video lkn ilibidi walipe mil 75 kama gharama za yeye kutokea kwenye video lkn WCB walitaka kutoa mil 50 ndipo aliposhauriana na uongozi wake na kuamua kukataa. "Ni kweli ningetokea kwenye video hiyo lakini walitoa pesa madafu,kaka mtangazaji siwezi kuuza sura kwa mil 50,ebu fikiria nimetumia karibia bilioni kutengeneza jina langu,nina biashara za mamilioni,leo Nassib anataka kunipa mil 50,that is not fair kwa kweli" Mdau yapi maoni yako kuhusu gharama za huyu mlimbwende?

Mke wa Boss Ananitega...

Image
Kibarua changu kipo hatarini kuota mbawa, anayeniponza ni mke wa boss. Boss wangu ni mtu mzima kidogo umri umeenda lakini mke wake ni kabinti kadogo alafu bado kabichi kabisa ni kabinti ambako saizi yake ni kijana mchapakazi kama mimi. Nimeingia kwenye mtihani mzito mimi ni Dereva mara nyingi huwa namchukua na kumpeleka anapotaka tukiwa wawili tu mimi na yeye nguo anazovaa ni full mtego naona hadi pichu ya jana nyeupe, ya leo nyekundu namuheshimu kama boss story anazoniambia ndio zilezile ivi unamke? Mara unamtoto, mara nihamie kwake, tukiwa tunakula mara anikanyage makusudi ilimradi tu visa. Sasa wikendi ndo ilikuwa balaa badala atoke na mumewe anatoka na mimi aliniambia nimpeleke akaogelee kufika huko ananiambia vua nguo tuoge. Jamaniii! Ni zaidi ya visa kibarua nakipenda lakini ndo hivyo kinaota mbawa. Nikimduu boss akijua si ataniua, achilia mbali kazi ishtoshe mzee mwenyewe pisto kiunoni

Basi la New Force Lapata Ajali na Kuua Watu 12

Image
Watu 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force kupinduka katika eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, Mkoani Njombe na kupelekea vifo hivyo pamoja na majeruhi. Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mkoa wa Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kumakia leo wakati likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe. Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na shirika la habari la taifa kutoka mkoani Njombe zinasema kati ya watu hao 12 wanawake ni nane akiwemo mtoto mmoja wa kike pamoja na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa kiume. Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka kabisa. Katika tukio lingine la ajali iliyotokea mkoani Kilimanjaro katika msafara wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki imesaba...