Mwenyekiti wa NCCR MAGEZI ahimiza watanzania kujenga Amani


Mwenyekiti wa Chama Cha NSSR-Mageuzi JAMES MBATIA amesema njia pekee kwa watanzania ya kujenga amani
Mwenyekiti wa Chama Cha NSSR-Mageuzi JAMES MBATIA
Mwenyekiti wa Chama Cha NSSR-Mageuzi JAMES MBATIA amesema njia pekee kwa watanzania ya kujenga amani ni kufanya kazi kwa bidii na kutenda haki katika maisha yao ya kila siku.

Katika mahojiano maalum na TBC jijini DSM kuhusu siku ya amani duniani MBATIA amesema ni muhimu kwa watanzania wakajijengea mioyo yao kuwa ya upendo na mshikamano ili kulinda amani iliyopo.

Naye Mhadhiri wa chuo cha Diplomasia, ISRAEL SOSTENES   amesema baadhi ya mila na desturi zinazochangia kutokea kwa migogoro katika bara la AFRIKAna kusababisha kukosekana kwa amani.
SOSTENES amesema mgawanyiko huo ulisababishwa  na historia ya ukoloni pia umezifanya nchi za AFRIKA zikose  misingi ya utawala bora wa kidemokrasia licha ya nchi hizo kupata uhuru.

Aidha SOSTHENES amesema tabia ya ubinafsi ya baadhi ya viongozi wa bara hilo ni sababu nyingine inayosababisha bara hilo kuwa na migogoro inayochangia kutokuwepo kwa mgawanyo sawa wa rasilimali za bara  hilo.

Siku ya amani huadhimishwa duniani kote  Septemba 21 kila mwaka

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU