Mzozo Kashmir: Pakistan yapiga marufuku filamu za India Image copyright AP Image caption Filamu za Bollywood zinazowashirikisha waigizaji maarufu kama Deepika Padukone, kulia, ni maarufu sana Pakistan Majumba makuu ya cinema nchini Pakistan yamepiga marufuku filamu za India, kama ishara ya kuonyesha umoja wao na vikosi vya Pakistan katika mzozo unaoshuhudiwa katika eneo la Kashmir. Marufuku hiyo imetangazwa katika miji ya Lahore, Karachi na Islamabad. Hatua hiyo inafuatia mzozo unaozidi kutotkota kati ya India na Pakistan. Siku ya Ijumaa, watayarishaji wa filamu kutoka India walipiga marufuku waigizaji wa Pakistan kufanya kazi Bollywood. Mwanasiasa mmoja wa mrengo wa kulia, amewaamrisha waigizaji wa Pakistan kuondoka India. Mhariri wa BBC kusini mwa bara Asia Charles Haviland anasema kwamba sio mara ya kwanza ambapo mzozo kati ya India na Pakistan umeathiri utamaduni wa mataifa hayo mawili. Mwandishi wa BBC anasema filamu za India ni maarufu sana Pakistan, kwani sekt...