Posts
Showing posts from July 31, 2016
Kala Jeremiah asimulia jinsi wimbo wake mpya ‘Wana Ndoto’ ulivyomtoa jasho (Video)
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Haikuwa rahisi kwa Kala Jeremiah kuikamilisha ngoma yake mpya, Wana Ndoto. Ni kwasababu wimbo huo aliurekodi mwanzo mwaka 2013 lakini producer aliyeutayarisha alishindwa kumkadhi. Baada ya kumpiga chenga kwa muda mrefu, rapper huyo alikata tamaa hadi mwaka 2016 alipopata mtoto, Alama. Amesema mtoto wake huyo alimpa tena hamu ya kuufanya tena wimbo huo lakini tatizo ni kuwa daftari lililokuwa na mashairi hakujua lilipo. Alilitafuta kwa zaidi kwa wiki mbili bila mafanikio lakini alikuja kulipata wakati akitafuta kitu kingine kabisa. Hata hivyo kazi nyingine ikaja kumpata Mtoto Miriam Chirwa aliyeimba chorus ya wimbo huu kwasababu alikuwa shule nje ya Dar. Ilimbidi amsubiri hadi afunge shule ndipo wakaingia studio kurekodi. Msikilize Kala akisimulia zaidi kwenye interview hii
Mambo 4 rahisi kuhamia Dodoma
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Kuchaa Barua pepe WAKATI watumishi wa umma wakikuna vichwa, kuhusu maagizo yaliyokwishatolewa na yanayoendelea kutolewa ya kutakiwa kuhamia Dodoma mara moja, taarifa zinaonesha kuwa gharama za kuhamia na kuishi, si kubwa kama inavyodhaniwa. Tathmini ya awali ya gazeti hili imeonesha kuwa hofu kubwa ya watumishi hao ni gharama za kuanza makazi mapya hasa nyumba na huduma za starehe na mapumziko baada ya kazi na wakati wa mwisho wa juma. Pia imebainika gharama nyingine ni mazoea tu, kwa kuwa huduma nyingi zikiwemo za chakula na usafiri, vimeonesha kuwa ni nafuu kwa mkoa huo, ikilinganishwa na mkoani Dar es Salaam. Takwimu za Gharama za Maisha (CPI) za Juni mwaka huu, zinaonesha kuwa sehemu kubwa ya kipato cha Watanzania sawa na asilimia 38, hutumika katika chakula huku hoteli na migahawa ambayo hutoa huduma hizo pia, pamoja na nyinginezo ikichukua asilimia 4.2 ya kipato cha Watanzania na kwa Dodoma huduma hizo ni rahisi kuliko Dar es Sal...
Zitto amuunga mkono Magufuli
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto 0 KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, amemuunga mkono Rais John Magufuli, kwa kuwakataza wafuasi wote wa chama hicho, kutojihusisha na maandamano ya aina yoyote kwa kuwa chama hicho hakijatangaza maandamano. Kauli hiyo ya Zitto, imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kuonya kuwa atakayethubutu kuandamana atakiona cha mtema kuni, huku Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, akitangaza kuwa maandamano ya wafuasi wa chama hicho nchi nzima, yako pale pale. Katika taarifa yake aliyotoa jana kwa vyombo vya habari, Zitto amesisitiza kwa wanachama hao na wafuasi wa chama hicho, kutojihusisha na maandamano ya aina yoyote kwa kuwa chama hicho hakijatangaza maandamano. Kauli hiyo ya Zitto ni pigo lingine kwa Chadema, ambayo juzi kupitia Mwalimu ilidai kupata barua za kuungwa mkono na taasisi nyingi katika maandamano hayo. Polisi Mwanzoni mwa Juni mwaka huu, Jeshi la Polisi nchini, kupitia kwa...
Kutizama Tv kunaweza kukuua, utafiti
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image caption Kutizama televisheni kwa muda mrefu ni hatari kwa maisha yako Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Japan umethibitisha kwamba kukaa kwa mda mrefu na kutazama vipindi vya televisheni kwa masaa mengi kunahatarisha afya kwani huhusishwa na maradhi yanasababisha mzunguko wa damu mwilini kutokuwa sawa. Watafiti hao wanasema, hali hiyo pia huenda ikasababisha damu kuganda na kutengeneza vidonge katika sehemu kama vile miguu, na iwapo mgando huo utasukumwa na nguvu za mzunguko wa damu na kuingia sehemu kama vile mapafu, husababisha vifo. Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku. Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miaka 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990. Matokeo yalikuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama televisheni, nayo hatari ya kupata ugonjwa huo wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40%. Image copyright THINKSTOCK Image caption Waliotaza...
Wanasayansi wagundua dawa kwenye pua ya mwanadamu
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Wanasayansi nchini Ujerumani wanasema wamegundua kwamba kuna chembechembe hai kwenye pua ya mwanadamu ambayo inaweza kutumia kuua viini hatari. Dawa nyingi za kuua viini vinavyosababisha maradhi hutolewa kutoka kwenye wanaoishi kwenye mchanga. Lakini kutokana na hali kwamba viini vinavyosababisha magonjwa mengi vimeanza kuwa sugu na kutosikia dawa, wanasayansi wamekuwa wakitafuta njia nyingine za kupata dawa mpya. Ripoti ya vipimo imebaini katika jarida la asili kwamba dawa aina ya Lugdunin, inaweza kutibu maambukizi ya maradhi yasiyosikia dawa. Watafiti katika chuo kikuu cha Tubingen nchini Ujerumani, waliogundua chembe hizo wanasema kuwa mwili wa binaadamu ni chanzo cha dawa mpya ambazo bado hazijatumiwa. Dawa ya mwisho kugunduliwa katika mwili wa binadamu ilipatikana mwaka 1980
Mugabe: 'Mtakiona' Trump akishinda
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image copyrig Image caption Robert Mugabe Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewaambia maseneta wa Marekani waliozuru taifa hilo kwamba watajutia kutofanya urafiki naye iwapo Donald Trump atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa mwezi Novemba. Maseneta hao Chris Coons na Adam Schiff waliambia gazeti la Politico nchini Marekani kwamba walikuwa katika taifa hilo kuzungumzia kuhusu usafirishaji wa wanyama mwitu na kwamba waliomba kukutana na rais huyo na wakashangaa kwamba alikubali kuonana nao. Maseneta hao wamesema kuwa Mugabe aliwataka kuelezea kwa nini Marekani inaliwekea vikwazo taifa hilo ambapo walitoa sababu kadhaa. Ni wakati huo ambapo bwana Mugabe aliwaambia: ''Wakati Trump atakapokuwa rais mutatamani mungefanya urafiki nami''