AFYA NA UZIMA

Kiufupi mimi ni mwanamke niliyeolewa miaka 5 iliyopita na kubahatika kupata watoto 2 wa kiume.
Mmoja ana 4 yrs na mdogo ana miezi 9.
Mume wangu yeye yuko Morogoro Manispaa anakofanyia kazi, na mara nyingi wakati wa weekend huja nyumbani Dar ili kujumuika na familia yake na wakati mwingine huwa ikitokea nafasi ya kuja Dar kikazi, basi huja kutuchungulia na kuendelea na shughuli zake.

Wakati najifungua huyu mtoto wangu wa pili, nilienda nyumbani kwetu Mwanza kumchukua mdogo wangu wa kike ili anisaidie kazi za hapa na pale wakati nikiwa kazini.
Na mtoto alipofikisha miezi 6, mdogo wangu aliniomba arudi Mwanza nyumbani ili akaendelee na masomo ya chuo.
Nilimkubalia na kumwambia kuwa kama atabahatika kunitafutia msichana wa kazi, nitamshukuru.
Baada ya kuondoka, kazi ikawa ni kutembea na yule mdogo kwenda nae ofisini huku mkubwa nikimpeleka Day care akashinde huko na kucheza.

Baada ya mwezi, mdogo wangu akaniambia kuwa amepata dada wa kazi na atakuja nae, nilishukuru sana na nikaanza maandalizi ya chumba cha kukaa msichana wa kazi.
Nilituma nauli na walikuja wote.
Baada ya kufika tuliongea kuhusu mshahara na taratibu zingine za kazi za pale kwangu.
Kisha baadae nikamuonesha chumba ambacho atakuwa anakitumia akiwa pale.

Tulikaa sebuleni tukipiga stori na muda wa kulala tuliagana vizuri, msichana akaenda chumbani kwake,mdogo wangu akaenda kwake nami nikaelekea kwangu.
Wakati nikiwa usingizini nikahisi sebuleni kuna watu wanaongea na kucheka...nikaamka ili nione ni nani wako sebuleni usiku ule, nikagundua kuwa ni mdogo wangu na yule dada wa kazi, wakasema wamerudi ili kuangalia tamthilia.
Sikutilia shaka, nikarudi zangu kulala.

Asubuhi kulipokucha msichana akaendelea na kazi zake kama kawaida na mdogo wangu akimsaidia.
Mwezi ulipita na nilipomuhoji mdogo wangu kuhusu chuo akawa ananiambia ataenda hivo nisiwe na shaka.
Basi nikaendelea na maisha yangu ila nilikuja kugundua ukaribu uliokuwepo kati ya mdogo wangu na msichana wa kazi.
Mdogo wangu ilikuwa akienda shopping huwa anamnunulia sidiria au chupi dada wa kazi, nikiuliza husema kuwa ameamua kumnunulia kama mwanamke mwenzake.
Sikutilia shaka japo niliona si hali ya kawaida kivile.
Baada ya tukio hilo ilipita siku kama 3 wakati naamka usiku nikaangalie milango kama imefungwa vizuri, wakati nakatiza sebuleni nikamuona msichana wa kazi na mdogo wangu wamekaa sebuleni wamelaliana kifuani.
Kwanza nilishtuka, mdogo wangu akasema, sio vibaya kumlalia mwanamke mwenzake kifuani.
Nikapita zangu nikarudi kulala.

Jumamosi moja mida ya saa 6 usiku, mume wangu alirudi toka Morogoro alichelewa maana gari ilipata pancha, alifika usiku na kwa vile simu yake iliisha chaji, aliamua kuzunguka dirishani kwangu ili anigongee...wakati anakatiza dirisha la msichana wa kazi, akasikia minong'ono na kilio cha mahaba cha kulalama.
Ilibidi aniamshe taratibu ili kama kaingiza mtu tujue.
Nilifungua mlango na kuzunguka dirishani, kweli nilisikia kilio hiko cha mahaba, yaani kama mtu yuko katika sex.
Basi tutaingia ndani na kwenda kumgongea mdogo wangu, tuligonga sana ila haukufunguliwa na tukaenda kwa msichana, alipofungua tukamuuliza mdogo wangu yuko wapi?
Akasema yuko kwake...tukaenda tena kugonga ila kulikuwa kimya.
Nahisi alijificha chumbani kwa msichana wa kazi.

Asubuhi kulipopambazuka niliwatuma gengeni wote, hapo sasa nikaingia kwa dada wa kazi kufanya upekuzi, tulipekua kila mahala kwa uangalifu na tulipofungua kabati tulikutana na kifaa cha kufanyia mapenzi pamoja na mafuta mbalimbali.
Baada ya hapo tukaenda chumbani kwa mdogo wangu, tukapekua kila mahala na tulipofunua begi lake, tukakuta picha za uchi za dada wa kazi na zingine wakiwa wamepiga huku wananyonyana maziwa, nyingine ni za aibu sana.
Kitandani kulikuwa na simu ya mdogo wangu, nikaichukua na kwebda kwenye gallery na kukuta picha za aibu na chafu.
Kumbe walikuwa wanashirikiana na mdada mwingine wa kazi wa jirani yangu.
Yaani sex group ya wanawake 3.
Kwenda kwenye message tukakuta mdogo wangu akimsifia dada wa kazi kuwa mtamu na anamkuna na kuahidi kutomuacha na hata dada mkubwa, yaani mimi nikimfukuza, basi lazima anifanyizie mimi au mwanangu.
Nilikaa chini na kuanza kulia, mme wangu akanibeba na kunipeleka chumbani.
Nikamuangalia mwanangu aliyelala kitandani haelewi chochote, huku akiwaziwa kufanyiwa kitu kibaya na mama yake mdogo.

Mpaka sasa mwanangu ana miezi 9 sasa, dada wa kazi yupo na mdogo wangu yupo...na mbaya zaidi mama ameniambia kuwa nimtafutie chuo huyu mdogo wangu hukuhuku Dar, asirudi Mwanza.
Niko njia panda, wanangu nawapenda, mdogo wangu nae nampenda, mie na mume wangu tumekosa cha kufanya.
Na msichana tangu afike pale...ni mchapa kazi na anawajali sana watoto na watoto wanampenda sana sana.
Niko njia panda, naombeni ushauri wenu

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU