Posts

Showing posts from September 25, 2016

Samsung kuuza tena Galaxy Note 7

Image
Image copyright AFP Image caption Takriban simu, Galaxy Note 7, milioni mbili laki tano zilirejeshwa kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, ili kupata btari mpya. Samsung imeanza mauzo ya simu yake, Galaxy Note-Seven nchini korea kusini, baada ya kusitisha mauzo yake mwezi mmoja uliopita, kutokana na madai kwamba simu hizo zinalipuka. Kampuni hiyo inasema hitilafu kwenye batri zake zilisababisha milipuko hiyo. Takriban simu milioni mbili laki tano zilirejeshwa kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, ili kupata btari mpya. Makampuni ya usafiri wa ndege yamekuwa yakiwaonya wateja wake dhidi ya kutumia simu hiyo ndani ya ndege. Hata hivyo sio simu zote zilizo na hitilafu kwenye batri zilizorejeshwa, na hivyo haijulikani wazi wakati marufuku ya kutumia simu hizo ndani ya ndege itakapoondolewa. Samsung inatoa simu za bure kwa wale walioathirika huku wafanyibiashara wa simu hizo wakipata mali mpya huku simu zaidi zikiendelea kufikishwa sokoni ''Tumetoa wito kwa waathiri...

Wenger: Wachezaji wa Afrika wamenifaa sana katika soka

Image
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Arsene Wenger ameongoza Arsenal kwa miaka 20 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameiambia BBC kuwa wachezaji kutoka nchi za Afrika wamekuwa wenye umuhimu mkubwa katika taaluma yake ya miaka 20. Wenga alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari kabla ya mechi ambapo pia alitunukiwa kwa kukiongoza klabu hicho kwa miongo mwili. Image copyright GETTY IMAGES Image caption Nwankwo Kanu wa Nigeria alikuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa wenye umuhimu mkubwa kwa Arsene Akiwa mwenye uso uliotabasamu, Wenger amesena kuwa wachezaji kutoa Afrika wana moyo, wenye ubunifu na nguvu, masuala ambayo ni vigumu kuyapa kwenye mchezo. Aliwataja wachezaji akiwemo Nwanko Kanu wa Nigeria, Kolo Toure wa Ivory Coast na gwiji raia wa Liberia George Weah, ambaye alikuwa meneja wake katika klabu ya Monaco nchini Ufaransa, kama wachezaji watatu waliokuwa na uswawishi mkubwa katika taaluma yake. Image caption Wenger akihutubia wanahabari...

Video ya raia wa Uganda akiuwawa na polisi Marekani yatolewa

Image
Polisi katika mji wa Marekani San Diego wametoa mkanda wa video ya mwanamme mweusi aliyepigwa risasi na kuuwawa na polisi siku ya jumanne. Image copyright REUTERS Image caption Waandamanaji, akiwemo Bi Agnes Hassan (aliyejifunga kitambaa kichwani), wakilalamikia kuuawa kwa Olango Video hiyo inaonyesha maafisa wawili wa polisi wakimkaribia Alfred Olango - mkimbizi kutoka Uganda - ambaye hakuwa amejihami, kabla ya mmoja wao kumfyatulia risasi katika mtaa wa El Cajon. Polisi wanasema kwamba mwanamme huyo alionyesha tabia potovu isiyoeleweka, japo mamake mzazi anasema alikuwa na matatizo ya kiakili na alifaa kupata usaidizi. Tukio hilo lilisababisha maaandamano makali katika eneo la El Cajon. Polisi huyo anaonekana akifyatua risasi mara nne, baada ya mwanamme huyo kuinua mikono yake hadi kwenye eneo la kifua, ishara ambayo polisi wanasema ilikuwa ya kujitayarisha kufyatua risasi. Video hiyo imetolewa baada ya siku tatu za maandamano makali , na katika mkesha wa siku ambayo famil...

Video ya raia wa Uganda akiuwawa na polisi Marekani yatolewa

Image
Polisi katika mji wa Marekani San Diego wametoa mkanda wa video ya mwanamme mweusi aliyepigwa risasi na kuuwawa na polisi siku ya jumanne. Image copyright REUTERS Image caption Waandamanaji, akiwemo Bi Agnes Hassan (aliyejifunga kitambaa kichwani), wakilalamikia kuuawa kwa Olango Video hiyo inaonyesha maafisa wawili wa polisi wakimkaribia Alfred Olango - mkimbizi kutoka Uganda - ambaye hakuwa amejihami, kabla ya mmoja wao kumfyatulia risasi katika mtaa wa El Cajon. Polisi wanasema kwamba mwanamme huyo alionyesha tabia potovu isiyoeleweka, japo mamake mzazi anasema alikuwa na matatizo ya kiakili na alifaa kupata usaidizi. Tukio hilo lilisababisha maaandamano makali katika eneo la El Cajon. Polisi huyo anaonekana akifyatua risasi mara nne, baada ya mwanamme huyo kuinua mikono yake hadi kwenye eneo la kifua, ishara ambayo polisi wanasema ilikuwa ya kujitayarisha kufyatua risasi. Video hiyo imetolewa baada ya siku tatu za maandamano makali , na katika mkesha wa siku ambayo famil...
Image
Serikali yaridhia ujenzi wa Bomba la Gesi HOIMA - TANGA SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongoza Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016 SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Magufuli. Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020. Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati...

Diamond Ataja Bei ya Kuuza Page yake ya Instagram Yenye Followers Milion 2

Image
AKIONGEA KUPITIA KITUO CHA TELEVISION CHA CLOUDS TV KUPITIA KIPINDI CHA SHILAWADU ,ALIULIZWA SWALI KUHUSU GHARAMA YA PAGE YAKE KAMA AKITAKA KUIUZA..BILA KUTAFUNA MANENO DIAMOND ALISEMA PAGE YAKE ANAWEZA KUUZA KWA BEI YA DOLA MILIONI 2 SAWA NA TSH BILIONI 4 ZA KITANZANIA.

Billnas Aungana na Nuh Mziwanda Kumvaa Petit Man

Image
Mwanzilishi wa kundi la LFLG rapa Billnas ameunga mkono tuhuma za Nuh Mziwanda kwa kumshukia meneja wao Petit Man juu ya uongozi mbaya na upigaji wa hela kupitia mgongo wao. Billnas akipiga story za eNewz na kusema kuwa matatizo ni kweli yametokea lakini akamshauri Nuh Mziwanda ni vyema kwa sasa wakatafuta namna ya kumaliza mzozo huo. "Petit ni mmoja kati ya watu wa LFLG, So kama mmoja wetu ana matatizo then wengine wanaweza kutumika kusuluhisha, au vinginevyo anaweza kupunguzwa ili wengine waendelee vizuri na kazi" aliongeza Billnas. Hapo awali mzozo kati ya Petit Man na wasanii anaowasimamia yaani Nuh Mziwanda na Billnas ulianza kusikika baada ya Nuh Mziwanda kujitoa chini ya usimamizi wa Petii Man kwa madai kuwa ni "mpigaji" na kwamba hutumia majina yao vibaya kupata pesa na pia si meneja anayewajali wasanii wake

JOTI TV/ KING CHIBA

Image

Alichofanya Mfakanyazi wa Shirika la Ndege la Ethiopia Alipookota Bahasha Yenye Milioni 21.8

Image
Shirika le Ndege la Kimataifa la nchini Ethiopia limempongeza hadharani mmoja wa wafanyakazi wake kwa kurejesha fedha kiasi cha dola elfu 10 (sawa ni shilingi milioni 21.8) zilizokuwa zimesahauliwa na mmoja wa abiria aliyekuwa kwenye ndege. Shirika la ndege la Ethiopia lilichapisha pongezi hizo kwenye ukurasa wake wa Facebook na kumpongeza mfanyakazi wa ndege hiyo Roza Shiferaw kwa kurudisha dola elfu 10 zilizokuwa ndani ya bahasha mali ya mmoja wa abiria. Shirika hilo liliongezea kuwa kitendo alichokifanya Roza ni ushahidi tosha kuwa shirika hilo lina wafanyakazi wenye maadili na heshima kwa wateja wao. Uongozi wa shirika hilo haukueleza zaidi kuwa abiria aliyesahau fedha hizo ni nani na mfanyakazi huyo alizikuta wapi.

Waziri Mkuu Kuhamia Dodoma Leo

Image
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajia  kuhamia rasmi Dodoma leo. Majaliwa anahamia mjini hapa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambako ndiko yaliko makao makuu ya nchi. Julai 25 mwaka huu, katika kilele cha siku ya mashujaa kilichofanyika mkoani hapa, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ifikapo Septemba mwaka huu, Serikali itakuwa imehamia mjini hapa. Hatua hiyo ya  waziri mkuu   ilitangazwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipozungumza  na waandishi wa habari. Alisema   Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili leo mchana akitokea   Dar es Salaam alikokuwa akiishi. “Baada ya kuwasili hapa  atafanya ziara ya siku mbili katika Manispaa ya Dodoma Oktoba mosi na Oktoba 2 mwaka huu   kukagua hatua mbalimbali za maandalizi ya kupokea   Serikali mkoani hapa. “Wakati wa ziara hiyo, atakagua majengo ya Serikali, maeneo ya kutolea huduma za afya, kituo cha umeme cha Zuzu, masoko, chan...

Chadema kutoa msimamo wa Oparesheni UKUTA Leo

Image
Mwezi mmoja baada ya Chadema kusitisha Operesheni Ukuta kupinga inachokiita ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia, leo inatarajia kutoa mwelekeo wa mkakati huo. Operesheni hiyo ilipangwa kuzinduliwa Septemba mosi nchini kwa maandamano na mikutano ya hadhara kama maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema, baada ya chama hicho kukumbwa na vikwazo kadhaa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara. Siku moja kabla ya kufanyika kwa operesheni hiyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuisitisha kwa mwezi hadi kesho, ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kusemezana na Rais John Magufuli na Serikali yake. Jana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema: “Kuhusu Ukuta, kesho (leo) tutatoa msimamo wetu juu ya kitu tutakachofanya.” Alisema operesheni hiyo ilisitishwa kutokana na sababu za msingi zilizoelezwa, hivyo kauli ya chama hicho leo itafafanua kwa kina kuhusu mambo yote yaliyojitokeza katika kipindi hicho ...

Viongozi mashuhuri wafika mazishi ya Shimon Peres

Image
Image copyright AFP Image caption Jeneza lenye mwili wa Peres limekuwa nje ya majengo ya bunge Jerusalem Viongozi mbalimbali duniani wanajiandaa kutoa heshima zao za mwisho wakati wa mazishi ya kiongozi shupavu wa Israeli marehemu, Shimon Peres, aliyefariki Jumatano wiki hii. Kuna ulinzi mkali katika eneo ambalo litatumika kwa mazishi yake, katika maeneo ya makaburi ya kitaifa mlimani Herzl mjini Jerusalem. Waombolezaji watajumuisha Rais wa sasa wa Marekani Barack Obama na Rais wa zamani Bill Clinton, aliyefanya kazi na Bw Peres katika mkutano wa mwafaka wa amani wa Oslo mwaka wa 1993. Rais wa zamani wa Israel Shimon Peres afariki Mchango wa Shimon Perez nchini Israel Viongozi kadhaa wa Kipalestina pia watahudhuria mazishi hayo akiwepo Rais Mahmoud Abbas na mpatanishi mkuu wa zamani Saeb Erekat. Itakuwa mara ya kwanza kwa Bw Abbas kuzuru Israel tangu 2010. Maelfu ya Waisraeli walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Peres, ambaye maiti yake imekuwa nje ya majengo ya Bung...