Mpiganaji wa Kiislamu kutoka Mali Al Mahdi afungwa jela ICC
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imemhukumu mwanamgambo wa Kiislamu raia wa Mali Ahmad Al Faqi Al Mahdi kifungo cha miaka tisa jela.
Al-Mahdi alikuwa ameshtakiwa makosa ya uhalifu wa kivita kuhusiana na kuharibiwa kwa makaburi tisa na msikiti mashuhuri katika mji wa kale wa Timbuktu, 2012.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake, Al Faqi Al Mahdi alikiri mashtaka.
Kesi dhidi yake ilisikizwa siku chache tu kwa sababu yake kukiri mashtaka.
Mshtakiwa ni mwalimu wa kidini na anadaiwa kuamrisha wapiganaji wa kundi la Kiislamu la
Ansar Dine waharibu turathi na maeneo ya kidini Timbuktu kati ya 2012 na 2013.
Comments
Post a Comment