Beki wa England John Stones, 22, ameiambia klabu yake ya Everton kuwa anataka kujiunga na Manchester City (Liverpool Echo). Image copyright GETTY Image caption John Stones anafuatiliwa na Man City Mshambuliaji Wilfried Bony, 27, anajiandaa kuondoka Manchester City, huku Galatasaray wakitoa pauni milioni 3 za kumsajili kwa mkopo (Sun), Leroy Sane, 20 anayesakwa na Manchester City, hajaiambia klabu yake ya Schalke kuwa anataka kuondoka, wakati meneja mpya wa City Pep Guardiola akiwa tayari kutoa pauni milioni 40 kumsajili kiungo huyo Mjerumani (Daily Star). Image copyright GETTY Image caption Fabregas kuungana tena na Mourinho? Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kumsajili kiungo kutoka Spain, Cesc Fabregas, 29, ambaye alikuwa naye Chelsea (Daily Mirror), Mourinho huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Newcastle, Moussa Sissoko, 26, iwapo atashindwa kumsajili Paul Pogba kutoka Juventus (Le 10 Sport), Man United wanaendelea kumfuatilia beki wa West Ham, Reece Oxfo...