Kimewaka Bavicha, Polisi Dodoma

Wakijiandaa Polisi wakijiandaa kuzuia vurugu mtaani
KATIKA harakati za kuhakikisha wafuasi wa vyama vya upinzani nchini zinazimwa, Jeshi la Polisi mkoani Dodoama limewatia mbaroni viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaandika Dany Tibason.

Waliokamatwa na jeshi hilo ni viongozi wa kitaifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) wakiwa wanakula na kunywa katika Bar ya Cape Town mjini humo.

Hata hivyo zoezi la kuwakamata viongozi hao linaendelea hata pale ambapo mtu yoyote anayeonekana kuwa, amevaa fulana zenye maneno yenye kaulimbiu za Chadema.

Tukio hilo limekuja ikiwa ni siku chache tangu jeshi hilo, kuzuia mahafali ya Umoja wa Wanavyuo Chadema (CHASO) kwa kuamuru wahusika waliokuwa wamekusanyika kwenye Hoteli ya African Dreems, mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kutawanyika.

Askari wenye mabomu ya machozi, silaha za moto na gari moja la maji ya kuwasha, walizunguka eneo la hoteli hiyo huku kiongozi wa polisi akitangaza;
“Ilani, ilani, imeamriwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, wote mliokusanyika mahali hapo mtawanyike, vinginevyo nguvu itatumika.”

Mahafali hayo hayakufanyika kwa wanavyuo na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani, kuondoka eneo hilo huku serikali mkoani humo ikieleza kuwa chanzo ni taarifa za uwepo wa ugonjwa wa ajabu, uliyodaiwa kuibuka wilayani Chemba na Kondoa.

Hata hivyo, siku chache baadaye, Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, alitangaza zuio la kufanyika mikutano ya kisiasa ya hadhara na ya ndani pamoja na maandamano akisema wakati wa uchaguzi umepita shughuli za kisiasa zipumzishwe mpaka kipindi cha uchaguzi ujao, ili watu wafanye kazi za maendeleo.

Akizingumza kwa njia ya simu leo Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, amethibitisha viongozi wa Bavicha kukamatwa wakituhumiwa kukusudia kuhamasisha kuikashifu serikali.

Amesema, hawatadhaminiwa mpaka Jumatatu, watakapofikishwa mahakamani.
Joseph Kasambala, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema-Taifa ametaja waliokamatwa kuwa ni Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha- Taifa, Julius Mwita, Katibu wa Bavicha -Taifa na George Tito, Mwenyekiti wa Bavicha mkoani Mbeya.

Akielezea ilivyotokea, Kasambala amesema, walikuwa katika ziara kwenye baadhi ya mikoa, walianzia mkoani Mara, katika Kijiji cha Mwitongo, Mwanza kabla hawajafika Dodoma juzi Saa 8:00 mchana.

Amesema leo walikusudia kukutana na vyombo vya habari mjini Dodoma, kuelezea hatua iliyofikiwa katika mpango wao wa Bavicha – Taifa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, kuzuia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya mkutano mkuu wa taifa, 23 mwezi huu.
Amesema, wakiwa Cape Town, majira ya usiku aliwaacha wenzake na kwenda kukutana na jamaa yake mwingine na kwamba baadaye alipata taarifa za wenzake kukamatwa na polisi.

Amesema kilichomsikitisha ni kukataliwa kuonana nao, alipofika kwenye kituo cha polisi cha kati jana asubuhi ambapo alitakiwa kwanza akaonane na viongozi wa polisi wa wilaya na mkoa (OCD, RPC).

Pia ameeleza kwamba, taarifa alizopatiwa kwenye kituo hicho cha polisi zimeeleza kuwa kosa wanalotuhumiwa kufanya ni kuikashifu serikali, kwa kuvaa T/shirt yenye maandishi “Dikteta Uchwara”.

Hata hivyo, Kasambara amesema, madai hayo ni ya uongo huku akionesha maandiko yaliyo kwenye fulana aliyokuwa amevaa, yenye rangi nyeusi na maandiko meupe yanayosema;
“Mwl. Nyerere; Demokrasia inanyongwa” upande wa mbele huku upande wa nyuma ikisomeka; “Haki na Amani.

Amesema, ziara yao inajumuisha viongozi sita wa Bavicha, akiwataja kuwa pamoja na yeye, watatu waliokamatwa ni Edward Simbeye, Katibu Mwenezi wa Bavicha–Taifa na Katibu wa Bavicha – mkoani Temeke, Hilda

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU