Posts

Showing posts from February 4, 2018

New Video: Msaga Sumu – Kitu Gani

Image
Msanii wa muziki wa Singeli Bongo, Msaga Sumu ameachia video ya ngoma yake mpya ‘Kitu Gani’. Itazame hapa.

Makonda Awawashia Moto Wakurugenzi

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewabadilikia Wakurugenzi mbalimbali wa halmashauri za wilaya mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa vitendo vyao vya kuwakaiimisha nafasi mbalimbali viongozi ambao hawana uwezo. Makonda amesema hayo leo Februari 10,2018 alipokutana na wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam ili kujibu kero na matatizo mbalimbali yanayowakabili ikiwa ni siku ya mwisho kwa zoezi la kupokea na kuzitafutia ufumbuzi kero hizo. Katika kusikiliza kero hizo baadhi ya watendaji wa Serikali walikuwa wakishindwa kujibu maswali ambayo Mkuu wa Mkoa alikuwa akiwauliza. "Mkurugenzi huyu mmempaje nafasi ya kukaimu, kwa hiyo Mkuu wa Idara anampa mtu ambaye hana uwezo kukaimu idara ili asipate idara si ndiyo maana yake? Maana huyu ndani tunatabia moja Mkuu wa Idara hana uwezo sasa hivyo anampa nafasi mtu ambaye hana uwezo ili yule mwenye uwezo asionekane, sasa huyu hana majibu anafanya nini hapa? Hajui lolote wala hana ripoti yoyote sasa Kukaimu kwake kumeishia kwenye huu...

Yanga Wamuweka Ngoma Kiporo

Image
Suala la mchezaji Donald Ngoma limebaki kiporo tena baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kushindwa kufikia maamuzi pamoja na siku za hivi karibuni kuahidi kulishughulikia. Akiongea leo Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema taarifa ya awali kutoka ofisi ya katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Mkwasa, kuwa suala la Ngoma linafanyiwa vikao jambo hilo limeshindwa kukamilika. ''Ukaribu wa michezo na majukumu mengi hapa katikati umefanya kushindikana kufikiwa kwa kile kilichokuwa kimepangwa au kulichotakiwa kujadiliwa kuhusiana na mchezaji huyo'', amesema. Aidha Ten pia ameongeza kuwa majeraha kwa wachezaji hayazuiliki na pia wapo wachezaji waliokaa nje kwa muda mrefu na wakarejea wakasaidia timu zao hivyo Donald yupo ni mchezaji wa Yanga mpaka hapo taarifa nyingine itakapotolewa. Kwa upande wake daktari wa timu hiyo Yanga Dr. Bavu amesema Ngoma ni miongoni mwa wachezaji wanne ambao bado ni majeruhi. Hivi karibuni Yanga walitoa taarifa kuwa wanasuburi ripoti ya dakata...

Uhalifu wa kimitandao unaweza kuangamizwa kwa njia gani Tanzania?

Image
 Tunaangazia zaidi uhalifu unaotekelezwa kwa kutumia simu za mkononi au rununu na mtandao. Polisi wanasema mwaka jana, makosa yaliyoripotiwa kwa polisi Tanzania ni zaidi ya 8,000. Je, uhalifu huu unaweza kuangamizwa?

Makamu rais wa Marekani agoma kula chakula cha jioni na dada rais wa Korea Kaskazini

Image
Makamu rais wa Marekani, Mike Pence amegoma kuwepo katika chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam. MATANGAZO Taarifa kutoka chombo cha habari cha Yo hap kimesema kuwa Pence alionana kidogo na bwana Kim wakati wakijaribu kukwepana kuonana uso kwa uso. Wakati huo huo, rais wa Korea ya Kusini Moon Jae-in ameshikana mikono na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un katika sherehe za ufumbuzi wa mashindano ya michezo ya Olympiki ya msimu wa baridi. Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. Pence alimleta Fred Warmbier kama mgeni Korea Kusini, baba wa kijana mdogo wa Marekani aliyekufa baada ya kutolewa gerezani huko Korea Kaskazini. Bwana Pence na Kim Yong-nam walikuwa wenyeji wa rais wa Korea Kusini kabla ya sherehe haijaanza huko Pyeongchang. Lakini Makamu rais wa Marekani alikaa kwenye tafrija hiyo kwa dakika tano tu na kuondoka. Katika ...

Huwa unanawa mikono kwa maji safi?

Image
Haba na Haba inaangalia unawaji wa mikono nchiini Tanzania, Je ni wakati gani unazingatia kunawa mikono na je unanawa na maji salama kiasi gani?