Baada ya Simu Kutoka kwa Rais Mwana FA Afunguka Haya
BAADA ya Rais Dk. John Magufuli kumpigia msanii Mwana FA na kupongeza wimbo wake, msanii huyo amesema ameguswa sana baada ya kupokea simu hiyo. Mapema wiki hii, Mwana FA alipigiwa simu na Rais na kumpongeza kwa kufanya vizuri katika nyimbo zake ukiwemo unaotamba ‘Dume Suruali’ na kusisitiza huwa anazisikiliza sana. Mwana FA amesema kuwa baada ya kupokea simu hiyo ameguswa sana na imempa kuzidi kujiamini kwa kazi anazozifanya. “Ukweli simu yake imenigusa sana, unajua unapoona hata viongozi wanapenda kazi zako ujue unakubalika sana, simu yake imenifanya nione bado nina jukumu la kuzidi kufanya kazi nzuri zaidi ya hapa,” alisema Mwana