Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU
Wewe kama mwanamme au mwanamke, najua unahitaji sana kulitunza penzi lako na kufanya lidumu milele kama wenyewe mnavyosema. Lakini wacha nikwambie kutunza penzi si ghalama kama watu wengi wanavyodhani, ila kuna vitu vichache ambavyo ukivifanya basi utadumu naye. Maana ingekuwa mapenzi ni ghalama basi maskini wasinge dumu kwenye mapenzi yao, lakini badala yake maskini ndiyo wanaongoza kudumu katika ndoa Na hizi ni hatua 10, ukizifanya mtadumu. (1) Kushukuru /Thanks You Kwa kawaida wasichana huwa wanapenda sana kusikiliza maneno yanayotoka midomoni, mwa wapenzi wao. Hivyo kumfurahisha mpenzi wake, ni lazima kumshukuru kwa chochote atakachokufanyia kwa kusema hasante, hata kama ukimtuma akakuletee soda kwenye friji, au kitu chochote, hata kama alichokuletea si sahihi kumkosoa papo hapo ni bora kumshuruku na kumwambia taratibu. KUWAPAMOJA / CROWD Mwanamke anapenda sana kuongozana na mpenzi wake...