Hatma ya Schweinsteiger Man United haijulikani

Image copyrightEPA
Image captionSchweinsteiger
Hatma ya mshindi wa kombe la dunia Bastian Schweinsteiger katika klabu ya Manchester United haijulikani kufuatia kuajiriwa kwa kocha Jose Mourinho .
Mourinho tayari amefanya usajili wa wachezaji watatu na sasa anamuandama kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba.
Schweinsteiger mwenye umri wa miaka 31,anaonekana kuwa mmoja wa wachezaji tisa ambao huenda wakaihama klabu hiyo.
Kiungo huyo wa kati ambaye ametangaza kustaafu katika soka ya kimataifa alifanya mazoezi pekee wakati ambapo wenzake walifanya zoezi pamoja kwa mara ya kwanza.
Image copyrightGETTY
Image captionMourinho
Washambuliaji Adnan Januzaj,Will Keane na James Wilson ,kiungo wa kati Andreas Pereira na mabeki Cameron Borthwic-Jackson,Tim Fosu Mensah,Tyler Blackett na Paddy McNair pia wameripotiwa kuondoka ijapokuwa wengine wataondoka kwa mkopo.
Kati ya wachezaji hawa hakuna hata mmoja aliyechaguliwa katika kikosi cha wachezaji 23 kwa mechi ya kirafiki siku ya Jumamosi dhidi ya Galatasaray mjini Gothenburg

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU