Posts

Showing posts from July 17, 2016

JOTI MUVI; MAFUTA LAINISHI

Image

Kikwete amkabidhi Magufuli 'majipu' ndani ya CCM

Image
Mwenyekiti mstaafu wa CCM Dkt Jakaya Kikwete, amekabidhi nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kwa Dkt John Pombe Magufuli, huku akimtaka kushughulikia baadhi ya mapungufu yanayokitia hasara chama ikiwemo kuokoa mali za chama. Kikwete ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Tanzania, ametoa hotuba yake ya mwisho kama mwenyekiti wa chama hicho leo katika mkutano mkuu maalum uliofanyika mjini Dodoma, na kutoa onyo kwa watu wote wanaoshikilia mali za chama kwa manufaa yao binafsi. Akitaja baadhi ya mali hizo, Jakaya Kikwete amesema kuna wanachama ambao wamejimilikisha viwanja vya chama hicho bila utaratibu rasmi na kuwapa tahadhari ya kuvirejesha katika chama haraka. Amemtaka mwenyekiti mpya mpya wa chama hicho kushughulikia suala la viwanja ambavyo bado havijapewa hati ili viendelezwe na kugeuzwa kuwa vitega uchumi na kuongeza wigo wa mapato ya chama. “Mkoa wa Dar es salaam pekee una viwanja 279 lakini ni 45 pekee ndivyo vina hati angalau UVCCM wanajitahidi kujenga majengo ya vitega uch...

TYPE UPSIDE DOWN

This link will direct you to make you tex upside down http://www.typeupsidedown.com
Image
How to type upside down Why would you want to type upside down? Put it in instant messages like MSN, AOL, gTalk Put upside down text on Twitter, MySpace, MSN Messenger, Facebook, YouTube Create very strong passwords Type upside down ... just for fun! �

Joe Budden aachia diss ya nne kwa Drake, ni baada ya kumkejeli kwenye ziara yake

Image
Bifu ya Drake na Joe Budden inaendelea kupamba moto. Alhamis hii Drake alimjibu kwa kejeli Budden kwenye ziara yake ya Summer Sixteen Tour. Alikuwa akitumbuiza huko Dallas. “We got that good energy going on,” alisema wakati wa show hiyo. “I should’ve brought Joe Budden up here to let him do ‘Pump It Up’ one time… F**k them ni**as, man.” Kufuatia maneno hayo ya Drake, Joe alitweet; HE WANT ATTENTION LOL.” Baada ya kuwa ameshaachia ngoma tatu za kumdiss Drake ‘Making a Murderer Pt. 1’, Wake na Afraidm, rapper huyo amedondosha diss nyingine aliyoipa jina, Just Because. Isikilize hapo chini.

Video: Diamond na Swizz Beatz wakutana na kuzungumza New York

Image
Producer huyo mkongwe, amewahi kupost video akifurahia nyimbo za wasanii wachache wa bara hili akiwemo Diamond. Na sasa wawili hao wamekutana jijini New York, Marekani. Staa huyo wa ‘Kidogo’ yupo nchini humo alikoenda kutumbuiza kwenye tamasha la One Africa Music na Swizz alihudhuria. Swizz alipata muda wa kwenda kusalimiana na Diamond backstage. Kwenye video zilizowekwa Instagram na Snapchat, Diamond anaonekana akimtambulisha Swizz kwa timu yake akiwemo Babutale, Dj D-Ommy na mtangazaji wa Clouds FM, B12 ambaye baadaye alimhoji. Tazama video hiyo chini.

Mrema Atoa Mpya 'Nawashangaa Wapinzani Mnavyozira Ovyo, Kwetu Anayezira ni Mwanamke, Wanaume Gani Nyie?'

Image
Mrema Afunguka: "Tarehe 16 Saa mbili asubuhi nilipigiwa simu na Rais Magufuli akanambia anataka kunipa kazi sikuamini, wala Mimi sikukataa kataa kama nikasema na iwe utakavyo Rais, Mbatia na wenzake walinichangia kama Mpira wa kona mwaka Jana, nashangaa wapinzani mnavyozira ovyo!! Kule kwetu Vunjo anayezira ni Mwanamke, nyie mnakimbia yule mama Bungeni ni Wanaume gani Nyie??" Mrema

NI NINI MAANA YA MAPENZI!

Image
Katika kuongelea suala zima la mapenzi ni vigumu kujua maana halisi ya mapenzi kwa maana halisi ya mapenzi ni kutokana na mtu mwenyewe anana vyoona. Lakini kwa ujumla mapenzi ni ile hali ambayo watu wawili wanaingia katika mahusiano ambayo yanabeba mambo mengi ikiwemo uvumilivu,kuchukuliana katika mambo yote yanayo husu maisha kwa ujumla. MSINGI HASA WA MAPENZ I 1-UVUMILIVU 2-HEKIMA 3-BUSARA 4-UPENDO 5-UWAZI 6-HESHIMA 1-Uvumilivu katika mapenzi ni suala la msingi sana kwani kama nilivyotangulia kusema kuwa mapenzi ni kama safari ambayo ina mambo mengi ikiwemo mateso na mabadiko mbali mbali. kwa hiyo bila uvumilivu ni kazi bure. 2-Hekima ni hali ya kunyenyekea. ili mapenzi yaweze kuwa mapenzi lazima kuwe na unyenyekevu wa kutosha.

Download hapa undergraduate guidebook

http://cas.tcu.go.tz/assets/images/Undergraduare_Admission_Guidebook_2016_2017.pdf

Video: TiĆ«sto ft. John Legend – Summer Nights

Image
TiĆ«sto and John Legend transport viewers to the Dominican Republic in the video for “Summer Nights.” Directed by Marc Klasfeld, the celebratory visual features jubilant scenes from the streets of Zona Colonial in Santo Domingo. Bike riders zoom in stuntman fashion, as beautiful women get ready for the night ahead. “It’s about to go down,” sings Legend.

Kati ya Wanafunzi 7,805 waliofukuzwa UDOM, ni 382 tu ndio wenye sifa

Image
Kati ya Wanafunzi 7,805 waliofukuzwa UDOM, ni 382 tu ndio wenye sifa Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi ambao watarejea kuendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya uchambuzi kumalizika na kupatikana idadi ya wanafunzi ambao wana sifa za kuendelea na masomo. Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa kwa kipindi chote walikuwa wakifanya uchambuzi ili kuona ni wanafunzi gani walikuwa na sifa za kusoma kozi hiyo maalum ambayo ilianzishwa kutokana na tatizo la walimu wa Sayansi. Alisema kuwa programu hiyo ilikuwa inahitaji walimu ambao watakwenda kufundisha shule za sekondari lakini kulikuwa na wanafunzi 1,210 ambao walikuwa wanachukua stashahada ya ualimu wa shule za msingi ambao ni kinyume na malengo na 6,595 wakichukua stashahada ya kufundisha shule za sekondari. “Baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, serikali ilifanya uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la ...

Madhara ya Kufanya Mapenzi au Tendo la Ndoa Mara Nyingi Kupita Kiasi

Image
Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono. Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.   Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari. Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.  Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile ...

Nyuki walazimu mechi ya kandanda kuahirishwa

Image
Image copyright BBC WORLD SERVICE Image caption Nyuki walazimu mechi ya kandanda kuahirishwa Mechi moja ya ligi kuu ya kandanda nchini Ecuador iliaahirishwa kwa dharura baada ya nyuki kuvamia uwanja. Amini usiamini mechi kati ya River Ecuador na Aucas katika jiji la Guayaquil ilisimamishwa baada ya nyuki waliokuwa wakipaa kutua uwanjani. Wachezaji kadhaa walidungwa na nyuki huku mashabiki wengi wakijeruhiwa. Wazima moto walilazimika kuingilia kati kujaribu kuwafurusha wadudu hao. Mechi hiyo iliyokuwa imechezwa kwa dakika kumi pekee ilisimamishwa kwa muda wa dakika 30 hivi, hata hivyo refarii katika mechi hiyo akaamua kuahirisha mechi iliyosalia

Donald Trump kugombea urais Marekani

Image
Image copyright REUTERS Image caption Donald Trump Donald Trump ateuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi November mwaka huu. Trump amepata uungwaji mkono na wajumbe kutoka majimbo na wilaya za Marekani katika kura mchujo wa kumpata mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama chake cha Republican kupitia mkutano mkuu wa chama chake mjini Cleveland. Baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais Donald Trump alitoa shukran zake kupitia mtandao wa twitter,na imetanabahishwa kwamba gavana wa jimbo la Indiana Mike Pence, ndiye mgombea mwenza .Taarifa zaidi zinasema watoto wawili wa Donald Trump wa kiume Donald na pia bintiye Tiffany wanatarajiwa kuhutubia mkutano mkuu wa wanachama wa chama hicho 

TCU kuanza kudahili wanafunzi wa kujiunga vyuo vikuu kesho

Image
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), itaanza kudahili wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kuanzia kesho. Akizungumza jana, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa Mollel alisema udahili kwa wenye diploma utaanza Julai 31. Dk Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa mwezi mzima ili kuruhusu wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili huo utafanyika kwa njia ya mtandao. Alisema ili wanafunzi waweze kuelewa programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume hiyo imeandaa maonyesho ya 11 yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22, mwaka huu. Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

JOH MAKINI FT CHIDINMA. PERFECT COMBO

Image

MJOMBA NISHAI. JOTTI VS KIPANDE

Image

DARASA. TOO MUCH

Image

MAKOMANDO. WANACHEZAJE

Image

Abakwa na watu 5 kwa mara ya pili India

Image
Image copyright REUTERS Image caption Binti huyo mwenye umri wa miaka 21 amebakwa na wanaume watano kwa mara ya pili. Kwa mtazamo wa wengi radi haiwezi kupiga mti mmoja mara mbili.,,, lakini kwa mwanamke mmoja nchini India hilo ndilo lililomkuta. Binti huyo mwenye umri wa miaka 21 amebakwa na wanaume watano kwa mara ya pili. Image copyright REUTERS Image caption Miaka mitatu iliyopita binti huyo alibakwa na wanaume wao hao watano katika mji wa Bhiwani. Miaka mitatu iliyopita binti huyo alibakwa na wanaume wao hao watano katika mji wa Bhiwani. Sadfa ni kwamba binti huyo aliyetorokea mji tofauti wa Rohtak ulioko katika jimbo la Kaskazini la Haryana alishikwa na kubakwa tena juma lililopita. Alikuwa akitembea barabarani kisha akatekwa nyara na watu ambao nusura wamnyonge. Alinusurika kufa lakini alichokipitia ni cha kutamausha sana. Image copyright REUTERS Image caption Binti huyo alibakwa kwa mara ya pili na kutupwa kichakani. Binti huyo alibakwa na kutupwa kichakani. Kwa ...

Akothee: Ana watoto watano lakini bado mbichi

Image
Akothee ni msanii mwenye watoto watano lakini bado ameonekana kuwa mrembo huku akidaiwa kuwa na mimba nyingine kwa sasa. Muimbaji huyo kutoka nchini Kenya ameonekana kuanza kuwapiga bao wasanii wengine kutoka nchi hiyo kutokana na juhudi anazozifanya kwenye muziki wake huku akiwa tayari ameshafanya collabo na mastaa wawili wakubwa Afrika, Diamond na Mr Flavour.Aidha Akothee aka Madam Boss ni mmoja kati ya wasanii wanaomiliki mkwanja mrefu zaidi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na biashara zake anazofanya ikiwemo ya kilimo na usafirishaj

Abiria washambuliwa kwenye Treni Ujerumani

Image
Image copyright EPA Image caption Mshambuliaji aliuawa alipokuwa akikimbia baada ya kutekeleza tukio hilo Mtu mmoja aliyekuwa na Kisu na Shoka amewashambulia abiria waliokuwa kwenye Treni Kusini mwa Ujerumani usiku wa jumatatu na kuwajeruhi watu wanne kabla yeye kupigwa risasi na Polisi na kufa alipokuwa akikimbia baada ya tukio hilo. Polisi wa mjini Wuerzburg wameeleza kwenye ukurasa wao wa Facebook kuwa abiria watatu wamejeruhiwa vibaya na wengine 14 wanapata msaada wa kitabibu kutokana mshtuko walioupata. Polisi wamesema bado hakuna taarifa yeyote kuhusu sababu ya kutekelezwa kwa shambulio hilo. vyombo vya habari vya Ujerumani vimemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya ndani mjini Bavaria kuwa mtu huyo ni mvulana wa miaka 17, mkimbizi mwenye asili ya Afghanistan. Mwaka jana Ujerumani iliwaandikisha wahamiaji milioni moja waliokuwa wakiingia nchini humo, zaidi ya 150,000 raia wa Afghanistan. Tangu mashambulizi ya hivi karibuni ya wanamgambo wa kiislamu nchini Ufaransa, ku...

Ugonjwa wa Kisukari ni Nini? Chanzo, Dalili na tiba yake

Image
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama ya moyo na mishipa ya damu, figo, saratani, kifua sugu, kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi kama vile ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell Disease). Ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya 2013, inadai magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio chanzo kikubwa cha vifo ulimwenguni, yakifanya asilimia 63 ya vifo vyote kwa mwaka. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza huua watu zaidi ya milioni 36 kila mwaka. Asilimia 80 ya vifo vinasababishwa na magonjwa hayo hutokea nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo. Inakisiwa kuwa mwaka 2020 magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na asilimia 60 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani. Nchini Tanzania, katika mpango wa upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukiza jijini Dar es Salaam, Mfuko wa...

Uhusiano Uliopo Kati ya Punyeto na Upungufu wa Nguvu za Kiume Kwa Mwanaume......

Image
 UKOSEFU  ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu. Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume. Ukisoma ...

Polisi 8,000 wasimamishwa kazi Uturuki

Image
Image copyright REUTERS Image caption Maafisa wa Polisi 8,000 wamesimamishwa kazi Uturuki Vikosi vya usalama nchini Uturuki vinasema kuwa zaidi ya maafisa 8,000 wa polisi wamefutwa kazi, kufuatia jaribio la mapinduzi lililozimwa wiki iliyopita. Runinga rasmi ya serikali nchini Uturuki- Anadolu, inasema kuwa maafisa wengine waliokamatwa ni pamoja na majenerali wakuu wa kijeshi. Takriban wanajeshi elfu 6,000 na wahudumu wa mahakama nao pia wamekamatwa. Image caption Fethullah Gulen amekanusha madai ya kuchochea mapinduzi Vyombo vya habari vinasema kuwa maafisa hao wanalaumiwa kwa kuwa na uhusiano na mapinduzi hayo ambayo serikali inadai kuwa yalipangwa na kiongozi wa dini aliyeko uhamishoni nchini Marekani- Fethullah Gulen. Msako dhidi ya maafisa wa usalama waliohusika na mipango ya kuipindua serikali juma lililopita nchini Uturuki, unaendelea. Image copyright REUTERS Image caption Kituo cha mafunzo ya wanajeshi wa angani mjini cha Istanbul, kilivamiwa na maafisa kukamatwa. ...