Video: Diamond akutana na mchekeshaji wa US, Kevin Hart
Diamond Platnumz ameianza vyema safari ya kutafuta tobo Marekani. Staa huyo ambaye yupo jijini Los Angeles, Marekani ambako tayari ameshoot video ya wimbo Marry You aliomshirikisha Ne-Yo, amekutana na mmoja wa mastaa maarufu sana Marekani. Amekutana na mchekeshaji na muigizaji wa filamu, Kevin Hart. Amepost kipande cha video Instagram akiwa na muigizaji huyo wa Central Intelligence anayesikika akiwasalimia followers wa Diamond. Kwa mujibu wa caption hiyo, inaonekana Diamond amefanya kazi na kampuni ya staa huyo, Hart Beat Productions