Saratani ya titi yampa umaarufu Instagram
Wakati alipokuwa akiugua saratani ya titi, Alison Habbal alikuwa akihisi kisunzi na kuchoka.
Akiwa miaka 36 wakati alipoanza kuugua ugonjwa huo, Alison ambaye ni raia wa Sydney alijua kwamba atapoteza nywele zake na titi lake.
Mpango wa kutengeza titi jingine kupitia upasuaji wa kutumia plastiki haukumvutia.
Sikutaka kuwekwa titi bandia kutoka kwa ngozi ya watu wengine ,niliona niweke tatoo ,alisema.
Wakati wote nilipokuwa mgonjwa niliwatafuta wachoraji tatoo katika mitandao,aliongezea.Na baada ya majadiliano marefu niliamua kumpa kazi ya uchoraji huo msanii kutoka New Zealand, Makkala Rose, mwenye umri wa mika 23 .
Tatoo hiyo ilichorwa mjini Melbourne kwa saa 13 mnamo tarehe mosi mwezi Julai.
Alison alifurahia kazi hiyo na akaamua kuchapisha picha yake katika mitandao ya Instagram na facebook.
Hatua ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa miongoni mwa wateja wa mitandao hiyo.Wengi walisifu wazo lake
Comments
Post a Comment