Posts

Showing posts from September 4, 2016

Video: Utani wa Stan Bakora baada ya Makonda kuagiza kupanda miti Oktoba 1

Image
Mchekeshaji Stan Bakora ameendeleza utani wake wa mitandaoni – sasa ni zamu ya kufuata agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alilolitoa kuhusu upandaji wa miti ifikapo Oktoba 1, mwaka huu. Tazama video hapo chini ya msanii huyo aliyoipost kwenye mtandao wake wa Instagram

Video: Michael Ross – Show Me Your Dance

Image

Video: Pipi ft Nikki wa Pili – Hafai

Image

Video: DJ Khaled Ft. Nas – Nas Album Done

Image

Video: TID ft Joh Makini – Confidance

Image

Real Madrid na Atletico Madrid zafungiwa na FIFA kufanya usajili hadi January 2018

Image
Klabu za Real Madrid na Atletico Madrid zinazoshiriki ligi ya Hispania, hazitaweza kusajili wachezaji kwa madirisha mawili ya usajili yajayo kufuatia FIFA kukataa rufaa yao waliyoikata juu ya kufungiwa kufanya usajili. Mwezi Januari mwaka huu kamati ya nidhamu ya FIFA ilitangaza kuzifungia klabu hizo zisifanye usajili katika madirisha mawili yajayo kwa kosa la kuvunja sheria za usajili waliposajili wachezaji chini ya miaka 18 wasio wahispania lakini adhabu hiyo haikuanza kufuatia timu hizo kukata rufaa na hivyo wakaweza kufanya usajili katika dirisha hili lililofungwa hivi karibuni. Hivyo baada ya rufaa zao kukataliwa miamba hiyo ya Hispania itaweza kusajili wachezaji wapya Januari,2018 na Atletico Madrid wanatakiwa kulipa faini ya pauni 622,000 na Real Madrid watalipa faini ya pauni 249,000. Lakini Real Madrid wamesema kuwa sasa wanaenda kukata rufaa ya katika mahakama ya michezo . Aidha klabu hizo zinaweza kusajili wachezaji lakini wasiwatumie. Barcelona April 2014 waliwahi ...

Maji ya mto yageuka 'rangi ya damu' Urusi

Image
Image copyright AFP/GREENPEACE Image caption Maji katika mto Daldykan yamekuwa ya rangi nyekundu Wachunguzi wa masuala ya mazingira nchini Urusi wanajaribu kubaini chanzo cha maji ya mto ulio karibu na kiwanda cha nikeli cha kampuni ya Norilsk Nickel yamebadilika rangi na kwua na rangi nyekundu. Picha za maji ya mto Daldykan ambayo yamebadilika rangi zimesambazwa sana katika vyombo vya habari Urusi. Gazeti la serikali la Rossiiskaya Gazeta linasema kuvuja kwa bomba la kusafirisha taka za mchanganyiko wa shaba nyekundu na nikeli huenda likawa kiini cha maji hayo kubadilika rangi. Norilsk Nickel ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa nikeli na palladium duniani. Image copyright SCREENSHOT Image caption Picha za runinga ya wizara ya ulinzi ya Zvezda TV Kampuni hiyo ina vinu na tanuri nyingi rasi ya Taimyr eneo la Krasnoyarsk katika jimbo la Siberia. Ujenzi wa vinu hivyo vikubwa ulifanyika enzi za muungano wa Usovieti. Kampuni hiyo ina kiwanda kwa jina Nadezhda karibu na mto Daldyk...

Korea Kaskazini yalipua bomu ‘sawa na la Hiroshima

Image
Image copyright EPA Image caption Mtangazaji wa TV ya Korea akitangaza habari za jaribio hilo Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini limesema taifa hilo limefanya majaribio ya bomu kupima uwezo wa bomu lake la nyuklia la kurushwa kwa kombora. Mlipuko wa bomu hilo umesababisha tetemeko la ardhi katika eneo lililofanyiwa majaribio. Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 5.3 kwenye vipimo vya Richter. Maafisa wa jeshi la Korea Kusini wanakadiria kwamba mlipuko huo ulikuwa sawa na wa kilo tani kumi za TNT, ukubwa sawa na wa bomu lililoangushwa Hiroshima na Marekani wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. Baadhi wanasema huenda bomu hilo la Korea Kaskazini likawa lilikuwa na nguvu ya kilo tani 20. Bomu lililoangushwa Hiroshima mwaka 1945 lilikuwa na nguvu ya kilo tani 15 (tani 15,000). Bomu lenye nguvu zaidi la nyuklia lililowahi kulipuliwa lilikuwa lile lililopewa jina Tsar-bomba, ambalo lililipuliwa na Urusi mwaka 1961. Image copyright REUTERS Image caption Korea Kaskaz...

JOTI NA ROLL CALL YA BWANA SHAMBA

Image

KR Mulla:Nipo Tayari Kurudi TMK Wanaume Family

Image
KR Muller amesema kama angetaka kurudi TMK Wanaume Family kwa Juma Nature angekuwa amerudi kwa kuwa hakuna aliyemfukuza. Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo ‘Rada Entertainment’ kwa TID, ameiambia Bongo5 kuwa bado anafurahishwa na maisha mapya ndani ya Rada Entertainment. “Mimi sijafukuzwa TMK, na pia naishi Temeke, kwa hiyo kama ningeamua kurudi TMK hakuna mtu ambaye angenifukuza kwa sababu sijafukuzwa,” alisema KR Madai ya Juma Nature kuwa KR ameharibikiwa toka ajiunge na Rada ya TID, rapa huyo amekanusha na kudai yupo vizuri kabisa tofauti na watu wanavyosema. “Kusema kweli mimi ni mtu mzima,na najitambua kwa hiyo swala la kusema TID ananiaribu siyo kweli kabisa,” alisema TID.

Amini adai kuukubali zaidi wimbo wake ‘Robo Saa’

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Amini Mwinyimkuu amedai kuukubali zaidi wimbo wake wa ‘Robo Saa’ kuliko nyimbo zake nyingine kwakuwa aliuandika kwenye mazingira magumu. Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha 5 Selekt cha EATV kuwa wimbo huo aliuandika wakati alipokuwa mkoani Lindi na hakuwa na uwezo mkubwa zaidi. “Wimbo huu nimeufanya kwenye mazingira magumu sana, nilikuwa siwezi kupiga guitar na niliuandika wakati nipo kijijini, Lindi nilipoenda kumtembelea mzee na hakukuwa hata na umeme,” amesema Amini. Msanii huyo ameongeza kuwa kwa sasa hayupo THT tofauti na watu wengi wanavyodhania ila muda wowote akipigiwa simu anajumuika nao. Kwa sasa Amini anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Hawajui’ aliouachia mwezi Mei mwaka huu

Mwanamke avunja rekodi ya ndevu ya Guinness World Record

Image
Image copyright PAUL MICHAEL HUGHES/GUINNESS WOR Image caption Harnaam Kaur anasema kwa miaka mingi amekejeliwa kwa sababu ya ndevu zake Mwanamitindo mwenye ndevu za urefu wa inchi sita ametambuliwa na Guinness World Record kuwa mwanamke wa umri mdogo zaidi duniani kuwa ndevu zilizokomaa kabisa. Harnaam Kaur, 24, ambaye ni mwanamke mtetezi wa kutambuliwa na kukubalika kwa hali ya mwili wa mwanadamu ulivyo bila ubaguzi anatoka Slough, Berkshire nchini Uingereza. Amesema ni heshima kubwa kwake kutambuliwa. Mzee wa umri wa miaka 145 Indonesia Ameeleza ndevu hizo ndefu kama sehemu ya juhudi zake za kukabiliana na watu wengi waliomkejeli kutokana na muonekano wake. Wengine waliotambuliwa kwenye rekodi za karibuni zaidi ni paka mrefu zaidi anayefugwa kama mnyama kipenzi pamoja na Ilama anayeruka juu zaidi. Image copyright PAUL MICHAEL HUGHES Image caption Machi 2016 Harnaam Kaur alikuwa mwanamke wa kwanza kushiriki maonyesho ya mitindo ya London Fashion Week akiwa na ndevu ...

Wanahabari nchini Kenya walaani dhuluma wanazofanyiwa

Image
Image caption Wamelalamikia kuhusu namna wanavyoshambuliwa na kupokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wanasiasa na umma. Waandishi wa habari nchini Kenya wameandamana Nairobi na miji mingine kupinga kile wanachosema ni kuongezeka kwa visa vya wanahabari kutishiwa na hata kuuawa. Maandamano yaliitishwa na Chama cha Waandishi wa habari ambacho kinasema wanahabari watano wamefariki katika hali ya kutatanisha katika kipindi cha mwaka mmoja. Maandamano yamefanyika siku kadhaa baada ya mwandishi wa habari za kisiasa kufariki katika mazingira ya kutatanisha eneo la Kilifi, pwani ya Kenya. Katika waraka wao walioutuma kwa bunge waandishi hao walilalamika kuhusu namna wanavyoshambaliwa na kupokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wanasiasa na umma. Image caption Wanahabari wamesisitiza kuwa wanayo haki ya kikatiba ya kutangaza taarifa. Wamesema baadhi ya viongozi wa kisiasa wa serikali kuu, kaunti pamoja na raia wamekuwa wakijiamulia wenyewe kuchukua sheria mkononi kuidhinisha mateso na kuwa...

Obama alipokutana na Duterte, kiongozi aliyemtusi

Image
Image copyright EPA Image caption Rais Obama na Rais a Ufilipino Rodrigo Duterte waangaliana Rais wa Marekani Barack Obama na kiongozi wa Ufilipino Rodrigo Duterte wamekutana ana kwa ana siku moja baada ya kiongozi huyo wa Ufilipino kuonekana kumtusi Bw Obama. Jumanne, Bw Obama alifutilia mbali mkutano uliokuwa umepangwa kati ya wawili hao baada ya Bw Duterte kumuita "mwana wa kahaba". Walikutana kwa njia isiyo rasmi muda mfupi kabla ya dhifa ya jioni ya viongozi wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia nchini Laos. Msemaji wa serikali ya Ufilipino alisema alikuwa na furaha sana kwamba mkutano huo ulifanyika. Obama afuta mkutano na kiongozi wa Ufilipino Mfahamu rais Duterte, kiongozi aliyemtusi Obama Maafisa wa Marekani walisema ulikuwa "mkutano mfupi" kabla ya dhifa iliyoandaliwa viongozi katika eneo la "kuketi viongozi". Bw Obama na Bw Duterte wanadaiwa kuingia kwenye ukumbi wa dhifa nyakati tofauti na hawakuzungumza au kukaribiana wakati wa h...