Posts

Showing posts from August 14, 2016

Olimpiki: Mwanariadha wa Kenya Apokonywa Medali Kwa Kosa la Udanganyifu

Image
Mwanariadha kutoka nchini Kenya aliyeshinda medali ya shaba kwenye riadha na kuruka vihunzi pamoja na maji, Ezekiel Kemboi amepokonywa medali yake kwa kosa la udanganyifu mchezoni kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea huko nchini Brazil. Kemboi (34) alimaliza kwenye nafasi ya tatu ya mashindano hayo ya kukimbia ya mita 3000 kwa kutumia muda wa 8:08.47. Ufaransa ilipinga ushindi huo wa Kemboi kwa kukata rufaa baada ya kubainika kuwa mwanariadha huyo wakati akiendelea na mbio hizo baada ya kuruka kiunzi na maji, alikanyaga nje ya mstari. Kamati ya mashindano hayo imekubali rufaa hiyo na kuamuru kumpatia medali hiyo ya shaba, Mahiedine Mekhissi kutoka Ufaransa aliyeshika nafasi ya nne baada ya kukimbia kwa muda wa 8:11.52. Hata hivyo Kemboi ambaye alikuwa bingwa wa mbio hizo kwenye mashindano ya Olimpiki ya 2012 ya nchini Uingereza amedaiwa kutangaza kustaafu kucheza mchezo huo.

Picha za Masanja na Mke wake Zazua Maswali Kwa Mashabiki wake..Wadai Mke wa Mchungaji Apaswi Kuvaa Hivyo

Image
Baada ya Harusi ya Mchekeshaji Masanja na Mkewe iliyofungwa Jumapili iliyopita wawili hao wameonekana kwenye picha mbali mbali wakijivinjari Honey Moon huku mavazi yao yakileta mabishano kama kweli ni Baba Mchungaji na Mama Mchungaji.... Baadhi ya Comments kwenye picha hizo hizi Hapa: "Wachungaji wa mwendo kasi.." "Kwa jinsi walivyovaa Biblia Takatifu inatufundisha kuwa utaweza kuwatambua kama ni nkweli wachungaji wa Kanisa la Mungu au watumishi wa kitapeli. Hivi vitu havijifichi. Mtumishi wa Mungu haachi maswali na hata akijifanya kwamba hamfahamu Mungu atajulikana tu kuwa ni mtumishi wa Mungu. Kumbuka Petro alipojaribu kusema hamfahamu Yesu na akaanza kuondoka ila waliokuwepo wakasema kuwa hata anavyotembea inadhihirisha yeye ni mtu wa Kristo. Je kwa muonekano wa Masanja, yeye ni mtumishi wa Mungu aliye hai????" "Don't judge by looks....THE LORD GOD ALMIGHTY knows the hearts of everyone" "Mavazi yanaonyesha uhalisia wa mtu. Kuna mavazi ambayo...

LIGI KUU VODACOM Mechi za Mwanzo Jumamosi Agosti 20

Image
Simba v Ndanda FC Stand United v Mbao FC Mtibwa Sugar v Ruvu Shooting Azam FC v African Lyon Majimaji FC v Tanzania Prisons Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, VPL, kwa Msimu mpya wa 2016/17 inaanza Leo kwa Mechi 5 huku Bingwa Mtetezi akianza utetezi wake Agosti 31 akirudi kutoka Lubumbashi. Wikiendi hii Yanga wanaruka kwenda huko Lubumbashi, Congo DR kucheza Mechi yao ya mwisho ya Kundi A la Mashindano ya CAF Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe wakiwa tayari wameeaga Mashindano hayo. Mechi hiyo itachezwa Jumanne Agosti 23. Kwenye VPL hii Leo, Simba SC iwataikaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam wakati Azam watakuwa Wenyeji wa African Lyon huko Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam. Huko Shinyanga ni Wenyeji Stand United wakicheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati Mtibwa Sugar wakiwa kwao Uwanja wa Manungu uliuoko Turiani, Mvomero mkoani Morogoro  kucheza na Ruvu Shooting ya Pwani na Tanz...

CARL GUGASIAN - The Friday Night Bank Robber.

Image
  Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17.  Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama 'The Frid ay Night bank robber'! Muhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber) Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'! Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio ...