LIGI KUU VODACOM Mechi za Mwanzo Jumamosi Agosti 20
Simba v Ndanda FC
Stand United v Mbao FC
Mtibwa Sugar v Ruvu Shooting
Azam FC v African Lyon
Majimaji FC v Tanzania Prisons
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, VPL, kwa Msimu mpya wa 2016/17 inaanza Leo kwa Mechi 5 huku Bingwa Mtetezi akianza utetezi wake Agosti 31 akirudi kutoka Lubumbashi.
Wikiendi hii Yanga wanaruka kwenda huko Lubumbashi, Congo DR kucheza Mechi yao ya mwisho ya Kundi A la Mashindano ya CAF Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe wakiwa tayari wameeaga Mashindano hayo.
Mechi hiyo itachezwa Jumanne Agosti 23.
Kwenye VPL hii Leo, Simba SC iwataikaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam wakati Azam watakuwa Wenyeji wa African Lyon huko Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.
Huko Shinyanga ni Wenyeji Stand United wakicheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati Mtibwa Sugar wakiwa kwao Uwanja wa Manungu uliuoko Turiani, Mvomero mkoani Morogoro kucheza na Ruvu Shooting ya Pwani na Tanzania Prisons ya Mbeya ikiwa Ugenini Uwanja wa Majimaji ya Songea kucheza na Majimaji FC ya huko.
LIGI KUU VODACOM
Jumapili Agosti 21
Kagera Sugar v Mbeya City
Jumatano Agosti 24
Toto Afrcans v Mwadui FC
Comments
Post a Comment