Chama cha ANC chaamua Zuma ni lazima aondoke
Chama tawala Afrika kusini African National Congress (ANC) kimemuomba rasmi rais Jacob Zuma ajiuzulu baada ya yeye kukataa kufanya hivyo mapema hii leo, taarifa zinasema. Taarifa kuhusu uamuzi huo umefuata mfululizo wa mazungumz ya maafisa wa juu wa chama hicho yalioendelea usiku kucha hadi kuamkia Jumanne alfajiri. Iwapo Bwana Zuma, mwenye umri wa miaka 75, hatoteteleka, atakabiliwana kura ya kutokuwa na imani naye bungeni ambayo anatarajiwa kushindwa. Akiwa amehudumu madarakani tangu 2009, ameandamwa kwa tuhuma za rushwa. Chama cha ANC hakijathibitisha rasmi mipango yake lakini duru kutoka cham hicho zimetoa ufafanuzi katika vyombo vya habari nchini Afrika kusini na pia kwa shirika la habara la kimataifa la Reuters. Rais Zuma amekiuka shinikizo linaloongezeka la kumtaka ajiuzulu tangu Desemba wakati Cyril Ramaphosa alipoichukua nafasi yake kama kiongozi wa chama cha ANC. Katibu mkuu wa ANC Ace Magashule ameiwasilisha barua kwa kiongozi huyo anayepigwa vita nyumbani kwake kati...