Posts

Showing posts from December 10, 2017

Mfumo wa sayari unaofanana na wetu wagunduliwa

Shirika la anga za juu la Marekani Nasa limegundua nyota ambayo inazungukwa na sayari nane, sawa na mfumo wetu wa jua ambao una sayari nane. Hiyo ndiyo idadi ya juu zaidi ya sayari kugunduiwa zikiizunguka nyota nje ya mfumo wetu wa sayari. Nyota hiyo iliyopewa jina Kepler-90, ina joto kiasi na ni kubwa kidogo kulishinda Jua. Awali, wataalamu wa anga za juu walikuwa wamefahamu uwepo wa sayari saba pekee zilizokuwa zinaizunguka. Lakini sasa wanasayansi wa Nasa wanasema wamegundua uwepo wa sayari nyingine ndogo iliyojaa mawe.