Posts
Showing posts from October 16, 2016
Mourinho: Tulidhibiti mechi na kuwanyamazisha mashabiki wao
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image caption Mkufunzi wa man United Jose Mourinho Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa timu yake ilidhibiti mpira pamoja na kufunga midomo ya mashabiki wa Anfield. Akihojiwa baada ya mechi hiyo iliotoka sare ya bila kwa bila,Mourinho amesema kuwa ijapokuwa hakutarajia matokeo hayo timu yake ilifanikiwa kuizuia Liverpool kwa kudhibiti mchezo kwa muda mrefu. ''Tulifanikiwa kudhibiti kelele za mashabiki wa Anfield pamoja na mchezo wa timu yao''. Mourinho amesema kuwa ijapokuwa wengi walidhani watashindwa timu yake iliodhibiti mpira na kuwapatia kibarua kigumu wapinzani wao. Hatahivyo mkufunzi huyo amekiri kwamba safu ya ushambuliaji ya Manchester United haikuwa imara wakati wa mechi hiyo. Image copyright GETTY IMAGES Image caption Man United ikichuana na Liverpool katika uga wa Anfield .Mechi hiyo ilikamilika katika sare ya bila kwa bila ''Hatahivyo nadhani hatukuimarika vilivyo katika safu ya mbele.Nashukuru kwamba pointi y...
Uislamu wapigwa marufuku Angola?
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image copyright OTHER Image caption Habari zisizokuwa za ukweli kuhusu Uislamu nchini Angola Ripoti za uongo kwamba Angola imekuwa taifa la kwanza duniani kupiga marufuku Uislamu zimezuka. Clare Spencer anauliza iwapo hilo linahusishwa na uchaguzi wa urais nchini Marekani.''Waislamu wamekasirika sana'' ,aliandika Frank Lea katika gazeti la Freedom daily. Angola kupiga marufuku Uislamu wanaodai ni madhehebu, na sio dini,ulielezea mtandao wa Libery Is Viral. Habari hiyo inatoa maelezo kuhusu msikiti unaovunjwa katika eneo la Zango lililo jirani na mji mkuu wa Luanda. Wanaona kile Waislamu wanavyowafanyia wale wasio Waislamu hususan barani Afrika,na wanachukua hatua kuzuia kutotokea hatua kama hiyo nchini Angola,habari iliochapishwa na mtandao wa ReaganCoalition.com. Pengine huenda Marekani wakajifunza moja ama mawili kutoka kwa Angola,liliongezea gazeti la America First Patriots,ambalo linasema misikiti 80 imevunjwa. Lakini habari hiyo sio ya kweli.Mtu mmo...
Mlo wa viwavi wazua vita vya kikabila DRC
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image caption Viwavi ni mlo mtamu katika eneo la Katanga nchini DRC Takriban watu 16 wameuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika vita vya kikabila huko mkoani Katanga ,kusini mashariki mwa taifa hilo kufuatia mgogoro wa kodi itakayotozwa viwavi. Viwavi huwa ni chakula cha raia wengi wa taifa hilo wanaoishi Magharibi mwa taifa la DRC karibu na eneo lililo karibu na mji mkuu Kinshasa,ambao uko maili kadhaa kutoka Katanga eneo lililozuka vita. Wadudu hao huchukuliwa kutoka kwa miti ,huchomwa na kuliwa na mchuzi.Viwavi hawawezi kusababisha vita katika taifa hilo hususan eneo la Katanga. Mkoa huo hujulikana kwa kupenda kula viwavi hao na watu hawajauwana kwa sababu yao hapo mbeleni. Lakini sasa kuna vita katika eneo hilo kati ya mbilikimo na makabila mengine. Mbilikimo ndio wanaotoka katika eneo hilo lakini wanahisi wamebaguliwa kwa kukosa mali asili na elimu. Kwa hivyo walipohisi kwamba chanzo kimoja cha mapato yao kinawekewa kodi,matokeo yakawa vita
Mtangazaji aliyemhoji Trump afutwa kazi
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image copyright AP Image caption Bw Bush ameomba radhi kutokana na aliyoyasema wakati wa mahojiano hayo Shirika la utangazaji la NBC nchini Marekani limemfuta kazi mtangazaji Billy Bush ambaye amekuwa akiendesha kipindi cha Today. Mgombea urais wa chama cha Republican alikuwa anahojiwa na Bw Bush miaka kumi iliyopita alipotoa matamshi ya kudhalilisha kuhusu wanawake. Ukanda wa mahojiano hayo yaliyofanyika mwaka 2005 ulifichuliwa majuzi na gazeti la Washington Post. Mke wa Donald Trump ajitokeza kumtetea Baada ya kufichuliwa kwa ukanda huo, viongozi wengi wakuu wa chama cha Republican walijitenga na Bw Trump ambayo yamezua utata. Kwenye video hiyo, Bw Bush anasikika akicheka baada ya matamshi ya Bw Trump. Billy Bush, 45, ambaye ni mpwa wa rais wa zamani George H W Bush, alikuwa awali amesimamishwa kazi baada ya kufichuliwa kwa video hiyo. Trump 'aliwapapasa wanawake kama pweza' Amekuwa mtangazaji wa kipindi cha Today kwa miezi miwili pekee. "Ingawa a...
Burundi yajiondoa katika mahakama ya ICC
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image copyright AFP Image caption Pierre Nkurunziza Taifa la Burundi hatimaye limekuwa taifa la kwanza kujiondoa rasmi katika mkataba wa Roma unaosimamia mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC. Hatua hiyo inajiri baada ya rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kutia saini sheria iliopitishwa na bunge pamoja na seneti ya kuiondoa Burundi katika mkataba huo. Wiki iliopita ,bunge la Burundi liliidhinisha mpango wa baraza la mawaziri kukata uhusiano na mahakama hiyo ya mjini Hague. Tayari mahakama ya ICC imeitaja mipango ya Burundi ya kujiondoa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC kuwa 'pigo' katika vita dhidi ya watu wasioheshimu sheria. Image caption Barua iliotiwa saini na rais Nkurunziza kuiondoa Burundi katika ICC Mwendesha mashtaka wa ICC alinukuliwa akisema kuwa atachunguza kile kilichotokea Burundi wakati wa maandamano dhidi ya rais Pierre Nkurunziza. Aliyekuwa waziri wa haki nchini Senegal Sidiki Kaba,ambaye anaongoza bodi hiyo ya...
Wanasayansi Kuanzisha Nchi Mpya Angani...Watu 50,000 Watuma Maombi Kuhamia Huko
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Wanasayansi hao wanataka kuunda taifa anga za juu ambalo litaitwa Asgardia Kundi la wanasayansi mjini Vienna, Austria wameanzisha mpango wa kuunda taifa la amani la aina yake ambalo litakuwa na jina Asgardia. Taifa hilo litaundwa katika anga za juu, eneo. Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo litakuwa nje ya udhibiti wa mataifa yoyote ya sasa na litakuwa katika mzingo wa dunia, eneo ambalo vyombo vya anga za juu huzunguka dunia. Wanasayansi hao wanapanga kurusha satelaiti ya kwanza, ya kuanzisha taifa hilo, mwishoni mwa mwaka ujao. Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja hivi karibuni watatambuliwa na Umoja wa Mataifa. Lakini baadhi ya wataalamu wanatilia shaka uwezekano wa mpango huo kufanikiwa ikizingatiwa kwamba sheria za kimataifa huzuia mataifa kudai umiliki wa maeneo anga za juu. "Raia" wa Asgardia, ambao watachunguzwa kwa makini kabla ya kukubaliwa, mwishowe watapewa hata pasipoti, anasema Lena d...
Rais MAGUFULI aongoza waombolezaji kumzika DIDAS MASABURI
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Rais DKT. JOHN MAGUFULI ameongoza viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa na wakazi wa jijini DSM katika kuuaga mwili wa meya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkwe wake Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho katika mwili wa Marehemu Didas John Massaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Rais DKT. JOHN MAGUFULI ameongoza viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa na wakazi wa jijini la DSM katika kuuaga mwili wa meya wa zamani wa jijini la DSM, Dkt. DIDAS MASABURI. Akizungumza katika viwanja vya KARIMJEE, Rais MAGUFULI amemwelezea Marehemu MASABURI kama mpiganaji mzuri wa Chama cha Mapinduzi. Mwili wa marehemu MASABURI unazikwa jioni ya leo katika eneo la Chuo cha ununuzi na ugavi-IPS kilichoko CHANIKA katika wilaya ya ILALA. Wakati wa uhai wake pamoja na mambo mengine Marehemu Dkt. MASABURI amewahi kushika nafasi mbalimbali kwenye Chama cha Mapinduzi-CCM, na serikalini, hivyo familia imeona ni...
MBUNGE wa BUKOBA ashikiliwa na polisi kwa kuandika barua ya kuomba misaada kwa wafadhilI
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Jeshi la Polisi Mkoani KAGERA limethibitisha kumshikilia na kumhoji Mbunge wa jimbo la BUKOBA Mjini WILFRED LWAKATARE kwa tuhuma za kuandika barua Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA AUGUSTINO OLLOMI Jeshi la Polisi Mkoani KAGERA limethibitisha kumshikilia na kumhoji Mbunge wa jimbo la BUKOBA Mjini WILFRED LWAKATARE kwa tuhuma za kuandika barua ya kuomba misaada kwa wafadhili mbalimbali ,kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani humo Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA AUGUSTINO OLLOMI uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo bado unaendelea . Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA AUGUSTINO OLLOMI amethibitisha jeshi la Polisi Mkoani KAGERA kumshikilia na kisha kufanya mahojiano na Mbunge huyo ambaye anatuhumiwa kuandika barua kwenda kwa wafadhili mbalimbali kuomba misaada kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi huku akijua kuwa suala hilo linaratibiwa na Kamati ya maafa ngazi ya taifa pamoja na kamati ya maafa ya mkoa wa Kage...
Mayanja akenua meno 32 Simba
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
KOCHA Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja NA SALMA MPELI, KOCHA Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amechekelea kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuwaacha mbali watani wao wa jadi, Yanga. Simba wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 23, wakifuatiwa na Stand United ambao wana pointi 20, huku Majimaji wakiendelea kuburuza mkia kwa pointi tatu. Akizungumza na BINGWA jana, Mayanja alisema wanafurahi kuendelea kupata ushindi katika mechi zao, kwani inaonyesha jinsi gani walivyojipanga kuchukua ubingwa msimu huu. “Tunashukuru kwa ushindi tunaoendelea kupata, lakini nitafurahi timu yetu kuendelea kuongoza ,” alisema Mayanja. Mayanja alisema kwa sasa wataendelea kukinoa kikosi chao ili kiweze kutisha zaidi katika mechi zitakazofuata dhidi ya Mbao, itakayochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam
Mrembo Atinga Global Afichua Siri Za ‘Scorpion’ VIDEO
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
KOFFI AOMBA RADHI HADHARANI
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Mwimbaji Koffi Olomide Achukua Dakika Moja Kuwaomba Msamaha Wakenya Kwa Kumpiga Mwanamke Mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide ambaye mwezi July aliwasili Nairobi Kenya akiwa na wanamuziki wake pamoja na dancers wake kwa ajili ya show na baadae kuripotiwa kukamatwa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike ni baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akifanya kitendo hicho. Koffi Olomide aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali, na hiyo ilielezwa kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kulikuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA. Baada ya kupita miezi kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo na Koffi Olomide kutowahi kujitokeza hadharani kulizungumzia, amejitokeza kupitia kipindi cha Television cha Churchill Show amewaomba msamaha wakenya na mashabiki wake kwa ujumla na kusema ……. ’ Kupitia Churchill show, nata...
China yatuma wana anga kwenye mzingo wa dunia
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image copyright AP Image caption Jin Haipeng (Kulia) na Chen Dong watakaa anga za juu siku 30 China imerusha roketi ambayo inawabeba wana anga wawili ambao wataenda kwenye kituo chake cha anga za juu kinachozunguka kwenye mzingo wa dunia. Wana anga hao waliondoka kutoka chumba cha kurushia roketi na satelaiti cha Jiuquan kaskazini mwa Uchina. Watatua katika kituo cha anga za juu cha Tiangong 2 ambapo watakaa siku 30, hicho kikiwa kipindi kirefu zaidi ambacho wana anga wa China wamekaa katika anga za juu. Mpango wa Marekani kupeleka watu Mars Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars Mwezi wa Jupiter 'unatoa michirizi ya maji' Uzinduzi huo na miradi mingine iliyozinduliwa awali ni ishara za kujiandaa kwao kutuma watu Mwezini au katika sayari ya Mars. Kituo cha awali cha anga za juu kilichoitwa Tiangong, Kasri la Mbinguni, kilifungwa mapema mwaka huu baada ya kupokea roketi tatu. Wana anga walio kwenye roketi iliyorushwa sasa ni Jing Haipeng, 49, ambaye amewahi kwe...
Stan Bakora Ajibu Mapigo Kwa Barakah The Prince
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Mchekeshaji maarufu Stan Bakora amefunguka juu ya povu lililomtoka Barakah The Prince siku kadhaa baada ya kuachia parody ya wimbo ‘Nisamehe’. Kupitia kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Stan amesema kuwa kama asingefanya vile video ingekuwa ya kawaida tu na isingeleta maana. Barakah ameshindwa kuelewa. Kama nisingefanya vile ile video isingeleta maana, lazima uonyeshe uhalisia. Kwani Baraka si mweusi kweli?,” amesema Stan. Stan aliendelea kwa kumtania Barakah kwa kumwambia kuwa hapa mjini [Dar es Salaam] ndio kwanza ana Christmas mbili. Awali baada ya Stan kuachia parody hiyo, Barakah aliandika kwenye Instagram: Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali.”
Mwanafunzi mmoja pekee apita mtihani Liberia
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image caption Darasa la shule moja nchini Liberia Ni mwanafunzi mmoja pekee nchini Liberia kati ya wanafunzi 42,000 waliokalia mtihani wa kila mwaka wa eneo la Afrika Magharibi aliyepita mtihani huo ili kujiunga na chuo kikuu. Armstrong Gbessagee mwenye umri wa miaka 18 kutoka chuo cha J.J Roberts United Methodist mjini Monrovia ndiye mwanafunzi wa pekee aliyefaulu. Amstrong alisema: Kokote unakotoka haimaanishi kwamba wewe sio mwerevu ukilinganishwa na watu wengine wa Afrika Magharibi.Natumai wengine wanaona ufanisi wangu kuwa motisha. Mitihani hiyo hufanyika nchini Ghana,Nigeria,Sierra Leone,Liberia na Gambia, mataifa yanayozungumza kiingereza. Mwaka 2013 takriban wanafunzi 25,000 walifeli mtihani huo wa kujiunga na chuo kikuu cha Liberia,ikiwa ni mojawapo ya vyuo vikuu vinavyoendeshwa na serikali. Rais wa Liberia Ellen Sirleaf Johnson aliitaja sekta ya elimu kuwa na tatizo.
SHILAWADU WAMPA MAKUVUUUUUUUUUUUUUU WOLPER
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Simu za Samsung Galaxy Note 7 ni marufuku Tanzania
- Get link
- X
- Other Apps
By
Unknown
-
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Samsung imesema haitaunda tena simu aina ya Galaxy Note 7 Tanzania na Rwanda zimepiga marufuku uingizaji, usambazaji na utumiaji wa simu za Samsung aina ya Galaxy Note 7. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya visa vya simu hizo kulipuka na kushika moto kuripotiwa nchi mbalimbali, jambo lililoifanya kampuni hiyo kutangaza haitaunda tena simu hizo. Aidha, Samsung iliwashauri wote waliokuwa wamenunua simu hizo kuzizima na kutozitumia tena. Nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zimefikia uamuzi huo katikati ya wiki iliyopita huku nchi nyingine kama Kenya zikisema hatua ambazo kampuni ya Samsung imezichukua hadi sasa zinatosha. Samsung: Zimeni simu za Note 7 ni hatari Rwanda yapiga marufuku Galaxy Note 7 Kwa mujibu wa gazeti la The East African, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano TanzaniaBw Innocent Mungy, amewataka wananchi wote ambao wamenunua simu hizo kuzizima na kuzirudisha katika maduka waliyonunulia na wauzaji hao kufuat...