Ligi Kuu Bara imeisha Yanga wakitwaa Ubingwa Azam FC na Simba zikishika nafasi ya pili na ya tatu, Nani anastahili kuwa mchezaji bora wa msimu?
Kampeni za 2015-16 Ligi Kuu zikiwa zimemalizika, ni wakati sasa wa kuamua nani anastahili kuwa mchezaji bora wa msimu. Ni mchezaji gani anastahili kupata tuzo ya mchezaji bora? Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Shomari Kapombe, Farid Mussa, Juma Abdul na Amissi Tambwe hali kadhalika na Aishi Manula wakiwa wameng'ara na mmoja kati yao anastahili kuwa mshindi. DONALD NGOMA Mzimbabwe huyu alianza msimu kwa kasi, amewashinda nguvu, kasi na maarifa mabeki wengi wa VPL msimu huu. Akicheza na Tambwe katika safu ya mashambulizi ya Yanga, Ngoma amefunga magoli 17 hadi sasa huku akisaidia magoli zaidi ya kumi. Amesabisha mikwaju mingi ya penalti kwa timu pinzani, pia walinzi wengi wamelambwa kadi nyekundu katika harakati za kumdhibiti mshambulizi huyo mwenye kukimbia kikakamavu. THABAN KAMUSOKO Mchezaji bora wa msimu? Inawezekana pia. Mzimbabwe huyo anakumbukwa kwa goli lake la dakika ya mwisho wakati Yanga ilipoifunga 1-0 African Sports katika game ya mzunguk...