HABARI.

Asilimia takriban 60 ya viumbe imeelezwa kupotea tangu mwaka 1970


Image captionAsilimia takriban 60 ya viumbe imeelezwa kupotea tangu mwaka 1970

Ripoti iliyochapishwa na muungano na makundi ya wanamazingira, WWF, na jamii ya wataalam wa wanyama huko London nchini Uingereza, imetahadharisha kuwa asilimia sitini ya wanyama imepotea kutokana na shughuli za kibinadamu tangu miaka ya 1970.
Ripoti hiyo ya viumbe hai imesema iwapo hali hii itaendelea jamii kubwa ya wanyama na misitu inayotegemewa maishani itapotea.
Watafiti wamechambua data zilizokusanywa kutoka kwa viumbe takriban elfu nne ya makundi mbalimbali ya ndege, samaki, mamalia, amphibia, na reptelia.
Ripoti hiyo iligundua kuwa mahitaji ya binadamu, yameongezeka mara mbili zaidi ikilinganishwa na nusu karne iliyopita, zaidi ikiwa ni katika chakula, msongamano na uharibifu wa mazingira ambayo viumbe wengine wanaishi

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU