Posts

Showing posts from August 21, 2016

Busu la Nelly Kamwelu shavuni kwa BABA TIFFAR akiwa na Wizkid

Image
Haipiti wiki bila Diamond kuwatoa povu mashabiki, hata kama alichokifanya si kwamba alidhamiria. Jumanne hii hitmaker huyo wa ‘Kidogo’ alipost video akiwa na starboy, Wizkid. Haijulikani wamekutana Dar au Afrika Kusini. Lakini video hiyo ilitafsiriwa vibaya baada ya Miss Universe 2011, Nelly Kamwelu, kutokea kusikojulikana na kumbusu Diamond shavuni. Haijulikani Nelly alikuwa mwenyeji wa nani, katika ya Diamond au Wizkid. Busu hilo limetafsiriwa vibaya na baadhi ya mashabiki wanaodai kuwa Diamond amemkosea heshima mpenzi wake Zari.. here we go again!

Wanaume ‘Wazaa’ Mapacha Watatu wa Kupandikizwa

Image
WANAUME wawili wanaoishi kama mume na mke (mashoga) nchini Afrika Kusini wanasemekana kuwa watu wa kwanza katika ukanda huo na huenda duniani kwa kuwa wazazi wa mapacha watatu, wawili wakiwa wanafanana, kwa kupitia mtu mwingine aliyebeba mimba. Wazazi hao ambao walikuwa majirani na mwanamichezo za zamani mlemavu, Oscar Pistorius, walikutana na mtu waliyempatia mbegu zao wakati wa mashitaka ya mauaji yaliyokuwa yanamkabili. Christo na Theo Menelaou wamewachukua watoto wao nyumbani kwao mjini Pretoria baada ya kukaa hospitali kwa wiki tatu za matatizo.  Kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati wao, Julai 2, mapacha hao walijikuta maisha yao yakining’inia kati ya uhai na kifo. couple (1)Joshua alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa njia ya upasuaji na ndiye alikuwa mzito kuliko wote akiwa na uzito wa kilo 1.8; Zoe alifuatia akiwa na kilo 1.3 na Kate aliyekuwa na kilo 1.3 pia. Watoto hao waliwekwa kwenye mashine za kuwasaidia kupumua hadi walipokuwa na nguvu za kutosha na kuwe...

Jifunze Haya Wewe Mwanamke Uliye Single

Image
1- Kamwe usisahau kumuomba Mungu wako kabla hujasema "YES" kwa yule unaedhani anapaswa kujenga maisha na wewe. Usikimbilie kuolewa. Kama utakimbilia kuolewa, utaikimbia ndoa na tena kwa majeraha makubwa. 2- Tambua lengo lako kabla hujaingia kwenye ndoa. Fanya biashara yoyote, tafuta shughuli ya kufanya. Usimsubiri mwanaume ndio useme unaanza maisha. Ongeza thamani ya maisha yako kwa kujenga maisha yako. 3- Usimkimbilie mwanaume kwa sababu ya pesa zake, magari, connection, cheo, kipaji, ucheshi, au background ya familia yake. Olewa na mwanaume aliye na hofu ya Mungu. Hapo utakua umekula BINGO...! 4- Jenga tabia ya kula vizuri kwa afya. Usile alimradi umekula. Kula vyakula vya kujenga mwili na uwe mlo kamili. Fanya mazoezi mara kwa mara kuepuka unene usio wa lazima. 5- Vaa vizuri. "first impression counts" hii inamaanisha kwamba muonekano wa mwanzo unamaana sana kwa mtu atakayekuona. Usiache maeneo yako ya siri yakaonwa na mwanaume yeyote, vinginevyo ut...

Askari Waliouwawa Dar na Majambazi, Adai ni Ishara Mbaya, Godbless Lema Afunguka

Image
Kwanza ninawapa pole familia za Polisi wote waliouwawa waliokuwa kwenye majukumu yao ya ulinzi wa raia na mali zao. Ni huzuni kubwa Polisi kuuwawa na silaha kwenda kwenye mikono ya wahalifu, tukio kama hili ni muhimu likatukumbusha kwamba Taifa linaweza kujengwa vyema kama kila mmoja atawajibika katika haki na sheria , kumbe Polisi wanaweza kuuwawa na Watu wasio na huruma na wasiotii sheria , kama ambavyo Polisi wasio na huruma na utii kwa Katiba wanavyoweza kujiandaa kuvunja ukuta unaotaka uwajibikaji wa matumizi sahihi ya Katiba na sheria. Ni ishara mbaya sana kuona walinzi wetu wanauwawa, lakini ni ishara mbaya zaidi kuona walinzi wetu wakiwa kwenye mazoezi hadharani ya kujipanga kudhibiti na pengine hata kuua Wananchi wanaodai haki yao Kikatiba ya mikutano ya vyama vya Siasa. Uimara wa Jeshi letu utajengwa na uhusiano mzuri kati yake na raia na sio silaha za kisasa na mazoezi ya vitisho hadharani. Poleni sana Watanzania kwa tukio hili baya, ni matumaini yangu kuwa wa...

Mr Blue: Jinsi Ndoa Yangu ilivyotaka kuvunjika

Image
Mr Blue amekiri kuwa skendo yake kuwa amekuwa akiwasiliana na ex wake, Naj ambaye kwa sasa ana uhusiano na Barakah Da Prince ilitaka kuivunja ndoa yake. Akiongea na Clouds FM, rapper huyo wa ‘Mboga Saba’ amedai kuwa mke wake, Wahyda sasa amekuwa na wivu wa kufa mtu tangu kuzuke skendo hiyo. “Sasa hivi naona kama wivu umezidi baada ya hii skendo ya hawa jamaa kuitengenezea kiki kwasababu wanataka kutoa nyimbo yao, skendo kwamba mimi nilimpigia yule mwanamke mwingine nani anaitwa, Najma yule. Wametengeneza kweli kabisa, mimi nimezipata za kunyapianyapia kwamba wametengeneza ili kukikisha nyimbo zao,” amesema Blue. “Lakini wamenikosea sana kwasababu wanataka kugombanisha ndoa yangu, mimi nina mke ujue, siwezi kumpigia mtu ambaye nimemwacha, ni kosa kubwa sana, halafu mke wangu yule ni mwanamke ambaye walikuwa watatu kupigania nani awe na mimi, yaani bora hata ningempigia mtu mwingine,” amesisitiza. “Ilifika karibu kama siku mbili tuna ugomvi mimi na mke wangu, ni kitu kikubwa sa...

Mke wa billionea Msuya apandishwa kizimbani

Image
Mke wa aliyekuwa bilionea wa madini maarufu jijini Arusha, marehemu Erasto Msuya, Miriam Msuya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. akikabiliwa na mashtaka ya kumuua dada wa bilionea huyo, Aneth Msuya. Mshtakiwa huyo akikabiliwa na mashtaka ya kumuua dada wa bilionea huyo, alifikishwa mahakamani hapo jana asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi huku baadhi ya ndugu waliokuwa katika eneo la Mahakama wakilia kwa uchungu mkubwa. Miriam Msuya ambaye alisomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali Diana Lukondo, mbele ya Hakimu Mkazi, Magreth Bankika. Naye Wakili Diana alidai kuwa, Mei 25, mwaka huu katika eneo la Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua Aneth Msuya ambaye ni wifi yake. Wakati huo mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka na kurudishwa rumande kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu, na pia kisheria mashitaka yanayomkabili hayana dhamana. Upande wa Jam...

Witness: Nimejichora tattoo kiunoni ili nisisaliti ndoa yangu

Image
Msanii hip hop hapa nchini, Witness aka Kibonge Mwepesi, ameitaja sababu ya kujichora tattoo ya jina la mpenzi wake Ochu Sheggy kwenye kiuno chake. Akiongea katika kipindi cha E-News cha East Africa TV, Witness amesema ameamua kufanya hivyo ili kuepuka kumsaliti mpenzi wake. “Ukiweka tattoo sehemu kama niliyoweka mimi(kiunoni) inazuia, hata unapotaka kumsaliti mwenza wako yule unayekuwa naye inamnyima hamu kabisa na anashindwa hata kukutamani tena,” alisema Witness. Pia Witness alisema kuwa watu wanadhani kuwa kuolewa ndiyo kumaliza kila kitu lakini kwa sehemu ambayo mapenzi yao yamefikia hakuna kitu ambacho anakihitaji tena kwakuwa mapenzi ni kuungana mkono na Ochu anamsaidia katika kila kitu anachofanya

Lady Jaydee: Fahamu muziki anaosikiliza, simu anayotumia na app anayoipenda

Image
Lady Jaydee ni shabiki pia wa muziki wa wasanii wengine. Akihojiwa na jarida la The Africa Report, Jaydee alieleza kuwa pale anapokuwa amekwama kwenye foleni, husikiliza nyimbo za wasanii kama Bruno Mars, Whitney Houston pamoja na muziki unaochezwa kwenye vituo vya redio. “Lakini nasikiliza aina mbalimbali ya muziki, hip hop, rnb, Jazz, afropop, muziki wa asili wa Tanzania, sina aina moja ya muziki wa kusikiliza,” alisema. Kuhusu simu anayotumia, Jide alisema anapenda iPhone 6s yake na kwamba app anayoipenda ni Beauty Plus anayodai huchukua picha vizuri na uwezo wa kuzitengeneza vyema

Timberlake avamia harusi ya watu bila mwaliko

Image
LONDON, England MWANAMUZIKI mahiri, Justin Timberlake, ametoa kali ya mwaka, baada ya kuibuka ghafla kwenye harusi bila mwaliko na kisha akapiga picha na wanandoa hao. Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita  katika mji wa New Hampshire  na kuwashangaza wanandoa hao ambao hawakuamini  kama aliyepo mbele yao ni staa huyo. Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya Habari, JT  alionwa na baba wa bibi harusi wakati akiwa katika matembezi yake kwenye hoteli ya Omni Mount Washington Resort na akamuomba kama angeweza kupiga picha ya pamoja na mahurusi jambo ambalo nyota huyo hakulipinga. Vyanzo hivyo vya habari vilieleza kuwa hali hiyo iliwashtua mno bwana  na bibi, Chelsey Gaudet na  Ryan Parks na waalikwa waliokuwapo eneo hilo na kuanza kujiuliza maswali. “Huyo ni nani?’ Alisikika mtu mmoja akihoji wakati  Justin akiwapongeza maharusi hao. Baada ya kupiga picha hiyo ya pamoja aliwaeleza kuwa alikuwa na harusi nyingine lakini anawapongeza ...

Timberlake avamia harusi ya watu bila mwaliko

Image
LONDON, England MWANAMUZIKI mahiri, Justin Timberlake, ametoa kali ya mwaka, baada ya kuibuka ghafla kwenye harusi bila mwaliko na kisha akapiga picha na wanandoa hao. Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita  katika mji wa New Hampshire  na kuwashangaza wanandoa hao ambao hawakuamini  kama aliyepo mbele yao ni staa huyo. Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya Habari, JT  alionwa na baba wa bibi harusi wakati akiwa katika matembezi yake kwenye hoteli ya Omni Mount Washington Resort na akamuomba kama angeweza kupiga picha ya pamoja na mahurusi jambo ambalo nyota huyo hakulipinga. Vyanzo hivyo vya habari vilieleza kuwa hali hiyo iliwashtua mno bwana  na bibi, Chelsey Gaudet na  Ryan Parks na waalikwa waliokuwapo eneo hilo na kuanza kujiuliza maswali. “Huyo ni nani?’ Alisikika mtu mmoja akihoji wakati  Justin akiwapongeza maharusi hao. Baada ya kupiga picha hiyo ya pamoja aliwaeleza kuwa alikuwa na harusi nyingine lakini anawapongeza ...

Belle 9 atinga kambi ya WCB, afanya mazoezi na Diamond

Image
Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii wa muziki wa R&B kutoka Morogoro, Belle 9 na yeye akasaini ndani ya label hiyo. Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Bugger Movie Selfie’ ameonekana akifanya mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB. Kwa mujibu wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Belle pamoja na Diamond wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku wakicheza. Hatua hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa kumuziki kuona huweza WCB ikamsaini msanii hiyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko. Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen Darli

TAZARA WAANDAA MAONYESHO MAALUM YA MIAKA 40 TANGU KUANZA SHUGHULI ZAKE

Image
Katika kuadhimisha miaka 40 Tangu kuanza kutoa Huduma kwa mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA,wameandaaa maonyesho maalum yatakayofanyika katika makao makuu ya mamlaka Hiyo Jijini Dar es salaam kuanzia Tarehe 24-26 ya mwezi huu yakiwa na lengo la kuonyesha huduma na utendaji kazi wake kwa kipindi chote cha utoaji wa huduma yao. Katika Taarifa iliyotolewa kwa wanahabari kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA Bwana Bruno Tandeo Chin’gandu  imeeleza kuwa katika maonyesho hayo watanzania watakaotemebea hapo watapata nafasi ya kujadili mijadala mbalimbali ikiwemo changamoto zinazokumba Sekta hiyo ya usafiri wa Reli nchini Tanzania ambapo wadau mbalimbali kutoka kila kona ya sekta hiyo watakuwepo kutoa Uzoefu wao juu ya maswala mbalimbali yakiwemo ya kisera,ya usafiri wa reli nchini. Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa maadhimisho hayo ya miaka 40 yamekuja ikiwa si tu Tazara kueleza changamoto zake bali yamekuja kipindi ambacho Tazara imekuwa ikipigana kuhakikisha kuwa ina...

Video: Wash Feat. Kevin Gates – Where You Been

Image
Kevin Gates is Wash’s wingman in the music video for their June collaboration “Where You Been.” Directed by Edward Tran, the sleek visual finds the duo in a nightclub surrounded by beautiful women. Wash sings and Gates raps, but both are out to take a lovely lady home with a series of questions.

Vyakula tiba kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo

Leo tutaangazia vyakula tiba kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo. Katika makala ya leo, tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa  wa vidonda vya tumbo (Ulcers)ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao. Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa huo unapaswa kujiepusha kula vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi. Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha. Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye caffeine, vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivyo kwani huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa. Kuna uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuk...

Utafiti: Je, wajua kuosha mdomo ni dawa ya kisonono?

Image
Image caption Dawa inayotumiwa kuosha mdomo Kuosha mdomo kunasaidia kupunguza maambukizi ya kisonono,watafiti wanaamini. Utafiti wa hivi majuzi umeonyesha kwamba binaadamu wanaweza kubeba magonjwa ya zinaa katika koo zao kwa mda wa wiki moja ama hata miezi bila ya kupata dalili zozote. Na wanaweza kusambaza kwa wengine kupitia ngono isio salama ya mdomoni. Wachunguzi wanajaribu kuona iwapo kuosha mdomo mara kwa mara kunaweza kusaidia kuzuia kuenea polepole na wataalam wanasema kuwa ni wazo ambalo linafaa kutumiwa. Image caption Ndani ya koo ya mdomo ndio eneo ambalo bakteria wa kisonono hukaa Kisonono husababishwa na bakteria na kinaweza kuishi katika koo,katika uume na uke na husambazwa kupitia ngono ya mdomoni pamoja na ile ya katika uke. Ugonjwa huo uliokuwa mwingi miaka ya 1950 umepungua baada ya dawa kugunduliwa

CHADEMA katika dhana ya kumtikisa Rais wa Tanzania

Image
Msingi wa kichwa cha mada yangu ipo kwenye kitabu cha Uongozi Wetu Na Hatima ya Tanzania kilichoandikwa mwaka 1994 na Mwl. Nyerere wakati taifa letu lilikuwa linakabiliwa na changamoto kadhaa za kihistoria ambazo ndizo zilimfanya kuingilia kati na kuandika kijitabu hiki ambacho kilikuwa kama nasaha, onyo, na usia kwa Watanzania. Mwl. Nyerere alisema, ‘’ huwezi kumtikisa Rais wa nchi bila kuitikisa nchi yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa wazi wazi na likaeleweka sawa sawa’’. Maneno ya Mwl.Nyerere yanatupeleka kwenye Sura ya Pili ya Katiba ya Tanzania 1977 Ibara ya 33(2) inayosema,‘’Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu’’. Ukubwa na umuhimu wa madaraka ya Rais wa Tanzania umeelezwa kwa kirefu katika sura ya pili kuanzia Ibara ya 33 mpaka 46. Akiandikia gazeti la “The London Observer” mwaka 1963, mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwa nafasi ya ‘Rais Mtendaji’ nchini, Mwl. Nyerere, aliwahi kukiri kuhusu madaraka makubwa ya Rais Kikatiba akis...

Video: Diamond Platnumz ft Psquare – Kidogo Dance ( WCB DANCERS )

Image

Mtikisiko mkubwa umekikumba chama cha wananchi CUF

Image
Mtikisiko mkubwa umekikumba chama cha wananchi Cuf kati ya wajumbe wa Tanzania bara na visiwani baada ya mvutano mkubwa wa kutaka kuwachagua viongozi wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na M/kiti wa zamani wa Cuf Prof.Ibrahim Lipumba pamoja na Makamu m/kiti visiwani Juma duni haji na kusababisha Mkutano huo Kuvunjika. Mvutano huo uliibuka baada ya wajumbe wa bara kuutaka Uongozi wa Cuf kumtaka Prof.Lipumba kufika katika mkutano huo na kutoa maelezo kuhusu kujiuzulu kwake,lakini pia baada ya kuwasili na kuingizwa na wafuasi wake kwa nguvu ukumbini zoezi la kumpa nafasi lilishindikana na wajumbe wakatakiwa kupiga kura na hali ilikuwa hivi. Nini hasa kiini cha kutotaka zoezi la kupiga kura na kusababisha wajumbe wote wa bara kutoka nje. Nje ya ukumbi makundi yanayomuunga mkono Prof.Ibrahim lipumba yalikuwa yakiendelea kupingana na mkutano huo lakini pia wengine wakijikuta wakipata vipigo hasa pale walipoonekana kumpiga Prof.Lipumba. Post navigati

Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa Afrika Kusini

Image
Image caption Bw Kibaki aliongoza Kenya kati ya 2002 na 2013 Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki, 84, amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini akipokea matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki. Kiongozi huyo wa zamani aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini Jumapili. "Aliandamana na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani hivi karibuni, na Wakenya watafahamishwa kuhusu hali yake wakati mwafaka," taarifa iliyotolewa na familia yake ilisema. Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu. Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu. Image copyright AFP Image caption Bw Kibaki na mkewe Lucy Mkewe, Lucy Muthoni Kibaki, alifariki Aprili mwaka huu akitibiwa jijini London

Rais wa Tanzania John Magu, baada ya kumuona wakati wa matangazo ya habari akitumia kwa umahiri mkubwa baiskeli ya kawaida. Katika taarifa iliyosomwa wakati wa matangazo ya habari, Rais Magufuli alisema kuwa atatumia pesa kutoka kwa mshahara wake mwenyewe kununua baiskeli hiyo na kumkabidhi mwanamme huyo baada ya juma moja

Image
Rais wa Tanzania John Magufuli ameahidi kuwa atamnunulia baiskeli ya magurudumu matatu, mwanamme mmoja mwenye ulemavu, baada ya kumuona wakati wa matangazo ya habari akitumia kwa umahiri mkubwa baiskeli ya kawaida. Katika taarifa iliyosomwa wakati wa matangazo ya habari, Rais Magufuli alisema kuwa atatumia pesa kutoka kwa mshahara wake mwenyewe kununua baiskeli hiyo na kumkabidhi mwanamme huyo baada ya juma moja

John Kerry aitaka Sudan Kusini kukubali wanajeshi 4000 wa UN

Image
Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry akiwa namwenzake wa Kenya Amina Mohamed Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry ameitaka Sudan Kusini kuwakubali wanajeshi 4000 wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Akizungumza baada ya kukutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mawaziri wa maswala ya kigeni jijini Nairobi,Kerry amesema kuwa Sudan Kusini inafaa kuheshimu makubaliano ya amani nchini humo kwa maneno na vitendo ili kuhakikisha kuwa yanaafikiwa. Amewataka viongozi wa taifa hilo kutojihusisha na vitendo vya ghasia ambavyo vinaweza kuchangia vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mapema mwezi huu Sudan Kusini ilisema kuwa haitashirikiana na Umoja wa Mataifa . Image caption Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Bwana Kerry pia amesema kuwa mafanikio makubwa yameafikiwa katika kukabiliiana na tishio la wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini Somalia,lakini mengi yanahitajika kufanywa katika eneo hili. Ameongezea kuwa Marekani itaahidi dola milioni 138...

Wema Sepetu ampigia magoti Idris Sultan

Image
Uhusiano wa Wema Sepetu na Idris Sultan unaanza kutukumbusha ule wa Chris Brown na Karrueche Tran ule wazungu wanauiita ‘off and on.’ Baada ya hivi karibuni kuzinguana tena hadi kumfanya Idris ajiondoe Instagram hadi sasa, wawili hao wanaonesha kuanza kutafuta suluhu. Wema amepost picha hiyo juu Instagram inayoonesha walikuwa wakiwasiliana kutumia app ya Facetime, aliandika:  That moment you realise how much u miss a special someone… Rudi basi… hata kidogo tu… 😔 Wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya Wema kuisusia show ya Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo wa Big Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika mwezi uliopita. Baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake kutompa support kwenye show zake, Idris naye aliamua kuipotezea show ya Usiku wa Vigoma iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo ndipo mambo yalipoharibika. Mashabiki wa Wema walikasirika baada ya shemeji yao kuikwepa show hiyo na wanamshambulia I...

UVCCM Waitisha Maandamano Nchi Nzima Agosti 31

Image
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano ya Amani nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo Amesema kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli. Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Aidha amesema kuwa katika maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Taarifa ya Polisi Dar kuhusu wanaojihusisha na ‘UKUTA’

Image
Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya maandamano ya nchi nzima Septembe 1 2016, Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limemkamata mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Yoram Mbyellah kwa kupatikana na kuuza sare aina ya fulana zenye maneno yanayodaiwa kuwa ni yakichochezi zikiwa na alama ya CHADEMA huku nyingine zikiwa na maneno ‘UKUTA’ Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema…>>>’August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ ‘ ‘Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake‘ –Kamanda Sirro ‘Ili tuishi kwa amani ni lazima tutii sheria na kama hutaki kutii sheria tutashughulika naye, Kama kuna ...