Mtikisiko mkubwa umekikumba chama cha wananchi CUF
Mtikisiko mkubwa umekikumba chama cha wananchi Cuf kati ya wajumbe wa Tanzania bara na visiwani baada ya mvutano mkubwa wa kutaka kuwachagua viongozi wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na M/kiti wa zamani wa Cuf Prof.Ibrahim Lipumba pamoja na Makamu m/kiti visiwani Juma duni haji na kusababisha Mkutano huo Kuvunjika.
Mvutano huo uliibuka baada ya wajumbe wa bara kuutaka Uongozi wa Cuf kumtaka Prof.Lipumba kufika katika mkutano huo na kutoa maelezo kuhusu kujiuzulu kwake,lakini pia baada ya kuwasili na kuingizwa na wafuasi wake kwa nguvu ukumbini zoezi la kumpa nafasi lilishindikana na wajumbe wakatakiwa kupiga kura na hali ilikuwa hivi.
Nini hasa kiini cha kutotaka zoezi la kupiga kura na kusababisha wajumbe wote wa bara kutoka nje.
Nje ya ukumbi makundi yanayomuunga mkono Prof.Ibrahim lipumba yalikuwa yakiendelea kupingana na mkutano huo lakini pia wengine wakijikuta wakipata vipigo hasa pale walipoonekana kumpiga Prof.Lipumba.