Askari Waliouwawa Dar na Majambazi, Adai ni Ishara Mbaya, Godbless Lema Afunguka

Kwanza ninawapa pole familia za Polisi wote waliouwawa waliokuwa kwenye majukumu yao ya ulinzi wa raia na mali zao.

Ni huzuni kubwa Polisi kuuwawa na silaha kwenda kwenye mikono ya wahalifu, tukio kama hili ni muhimu likatukumbusha kwamba Taifa linaweza kujengwa vyema kama kila mmoja atawajibika katika haki na sheria , kumbe Polisi wanaweza kuuwawa na Watu wasio na huruma na wasiotii sheria , kama ambavyo Polisi wasio na huruma na utii kwa Katiba wanavyoweza kujiandaa kuvunja ukuta unaotaka uwajibikaji wa matumizi sahihi ya Katiba na sheria.

Ni ishara mbaya sana kuona walinzi wetu wanauwawa, lakini ni ishara mbaya zaidi kuona walinzi wetu wakiwa kwenye mazoezi hadharani ya kujipanga kudhibiti na pengine hata kuua Wananchi wanaodai haki yao Kikatiba ya mikutano ya vyama vya Siasa.

Uimara wa Jeshi letu utajengwa na uhusiano mzuri kati yake na raia na sio silaha za kisasa na mazoezi ya vitisho hadharani.

Poleni sana Watanzania kwa tukio hili baya, ni matumaini yangu kuwa watu hawa watatiwa nguvuni haraka iwezekanavyo

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU