Timberlake avamia harusi ya watu bila mwaliko

LONDON, England
MWANAMUZIKI mahiri, Justin Timberlake, ametoa kali ya mwaka, baada ya kuibuka ghafla kwenye harusi bila mwaliko na kisha akapiga picha na wanandoa hao.
Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita  katika mji wa New Hampshire  na kuwashangaza wanandoa hao ambao hawakuamini  kama aliyepo mbele yao ni staa huyo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya Habari, JT  alionwa na baba wa bibi harusi wakati akiwa katika matembezi yake kwenye hoteli ya Omni Mount Washington Resort na akamuomba kama angeweza kupiga picha ya pamoja na mahurusi jambo ambalo nyota huyo hakulipinga.
Vyanzo hivyo vya habari vilieleza kuwa hali hiyo iliwashtua mno bwana  na bibi, Chelsey Gaudet na  Ryan Parks na waalikwa waliokuwapo eneo hilo na kuanza kujiuliza maswali.
“Huyo ni nani?’ Alisikika mtu mmoja akihoji wakati  Justin akiwapongeza maharusi hao.
Baada ya kupiga picha hiyo ya pamoja aliwaeleza kuwa alikuwa na harusi nyingine lakini anawapongeza ingawa aliingilia shughuli yao bila mwaliko

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU