Lady Jaydee: Fahamu muziki anaosikiliza, simu anayotumia na app anayoipenda
Lady Jaydee ni shabiki pia wa muziki wa wasanii wengine.
Akihojiwa na jarida la The Africa Report, Jaydee alieleza kuwa pale anapokuwa amekwama kwenye foleni, husikiliza nyimbo za wasanii kama Bruno Mars, Whitney Houston pamoja na muziki unaochezwa kwenye vituo vya redio.
“Lakini nasikiliza aina mbalimbali ya muziki, hip hop, rnb, Jazz, afropop, muziki wa asili wa Tanzania, sina aina moja ya muziki wa kusikiliza,” alisema.
Kuhusu simu anayotumia, Jide alisema anapenda iPhone 6s yake na kwamba app anayoipenda ni Beauty Plus anayodai huchukua picha vizuri na uwezo wa kuzitengeneza vyema
Comments
Post a Comment