Posts

Showing posts from June 19, 2016

Mtanzania aajiriwa na klabu ya Dubai

Image
Mwanariadha wa Tanzania katika eneo la Mianzini,huko Arusha amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Al Nasri ya Dubai kuiwakilisha kwa shindano la miruko mitatu yaani triple jump. Asema mfuko wake sasa una uzito tofauti na miaka iliyopita akisota mjini Arusha. ''Nimezaliwa Arusha miaka 22 iliyopita.Nilianza kushiriki mashindano ya shule mwaka 2011''. Pia anasema kuwa ameshiriki mashindano ya taifa kuanzia mwaka 2011 na kuwa bingwa mara zote katika michezo ya triple jump na long juu Mwanariadha wa Tanzania katika eneo la Mianzini,huko Arusha amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Al Nasri ya Dubai kuiwakilisha kwa shindano la miruko mitatu yaani triple jump. Asema mfuko wake sasa una uzito tofauti na miaka iliyopita akisota mjini Arusha. ''Nimezaliwa Arusha miaka 22 iliyopita.Nilianza kushiriki mashindano ya shule mwaka 2011''. Pia anasema kuwa ameshiriki mashindano ya taifa kuanzia mwaka 2011 na kuwa bingwa mara zote katika michezo ya triple j...

Mchezaji aadhibiwa kwa kutoa hewa chafu

Image
Refa mmoja raia wa Sweden, alimpa kwa mpigo kadi mbili za njano mwanasoka Adam Lindin Ljung-kvist, akiwa uwanjani, kwa kosa la kutoa hewa mbaya. Mchezaji huyo alipokuwa katika harakati za kushangaa kuhusiana na hatua ya refa huyo, alipigwa kadi nyekundu na kuondolewa uwanjani. Refa huyo ametaja kitendo cha Adam cha kutoa ushuzi , kama tabia isiyo ya mchezaji. Lakini kulingana na Adam, alidhani alikuwa akifanya hivyo kimaumbile tu na wala hakuwa na nia ya kumchafulia refa hewa. Taarifa hiyo imeibua malumbano makubwa kote duniani katika mtandao wa kijamii, huku wengine wakisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji soka kupigwa kadi nyekundu kwa sababu ya kuchafua hewa. Amesema kuwa ameshangazwa sana na refa kumtimua, huku akiongeza kuwa, kocha na wachezaji wenzake hawakuamini walipomuona akirejea katika eneo la wachezaji wa ziada na kuwaambia kuwa amepigwa kadi nyekundi kwa "kushuta." Adam, mwenye umri wa miaka 25 anaichezea timu ya Pershagen SK, inayo burura mkia katika l...

Mataifa 6 ya EU kujadili mustakabali wao

Image
Mataifa 6 waanzilishi wa Muungano wa Ulaya EU wanakutana leo kujadili mustakabali wao wa baadaye baada ya Uingereza kuamua kujiondoa kutoka kwa muungano huo. Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, ufaransa,Italy, Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi wanatarajiwa kuanzisha mchakato huo pasi na kuwa na ngoja ngoja. Tayari rais wa tume ya muungano wa Ulaya , Jean-Claude Juncker, amesema anataka kuanzisha majadiliano mara moja ya jinsi Uingereza itakavyotoka rasmi kutoka EU . Bw.Juncker amesema haieleweki kwamba swala hilo likumbwe na hadi waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ang'atuke kutoka madarakani baada ya kushindwa katika kura hiyo ya maoni iliyoamua nchi hiyo ijibandue kutoka Umoja wa Ulaya. Mawaziri hao pia wanatarajiwa kuweka masharti mapya yatakayowazuia wanachama wengine kuiga mfano wa Uingereza,baada ya vyama vya mrengo wa kulia katika mataifa mengi duniani kupongeza uamuzi huo wa Uingereza kujitoa kutoka muungano wa Ulaya... Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Ujeruma...

SHILOLE AJA NA MAPYA

Msanii wa muziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameanzisha label yake mpya ‘Shilole Entertainment’ ambapo pia amemsaini msanii chipukizi aitwae ‘Amaselly’. Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘SayMyName’, amekiambia kipindi cha Clouds E kinachoruka katika runinga ya Clouds TV, kuwa ameamua kuanzisha label hiyo ili kuwasaidia wasanii wenye vipaji lakini hawapati nafasi. “Yeah nimemsani Amaselly aka Gaucho, kwa sababu ni msanii mwenye heshima, amenitafuta kwa muda mrefu, Shilole nisaidie nisaidie, kwa hiyo nikajifikiria, nikaamua kumsaidia,” alisema Shilole Pia Shilole amesema amemsaini msanii huyo kupitia label yake mpya iitwayo Shilole Entertainment. Kwa upande wa Amasely alimshukuru Shilole kwa uwamuzi wa kumsaidia huku akihaidi mambo mazuri.