Posts

Showing posts from September 11, 2016

Video: Flavour – Obianuju

Image
Msanii toka Nigeria

Mrema ayaomba makanisa kutenga sadaka za Jumapili moja kuwatoa wafungwa gerezani

Image
Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa, Augustino Mrema ameyaomba makanisa nchini kutenga sadaka ya Jumapili moja kama harambee kwaajili ya kuwatoa baadhi ya wafungwa gerezan Mrema ametoa pendekezo hilo, Alhamis hii. “Ninachosema ifanyike harambee kwenye makanisa yote, tuangalie siku moja jumapili,wachungaji na maaskofu hizo sadaka msiwe mnazichukua tu ,chagueni Jumapili moja tu katika sadaka nyingi mnazokusanya, Jumapili moja sadaka zinazopatikana kwa siku hiyo zitumike kuwalipia faini wafungwa. Na baadhi ya waliofungwa ni wakristo wenu sio wapagani walioko magerezani, maana watu wanaweza wakachekelea wakifikiri sijui nini, ni wakristo waliobatizwa kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu, wakianguka kwenye dhambi wanapelekwa pale,” alisema. “Ni kosa kwa mchungaji kuwa na mkristo yupo ndani kwa kushindwa kulipa faini ya shilingi elfu 50 anaendelea kusota, kwahiyo natoa wito hiyo sadaka isaidie kutoa wafungwa gerezani, ni pendekezo sio lazima wala sina uwezo wakuwaaamrisha...

Hatuna mpango wa kufanya video ya Hands Up ya Young Dee – MDB

Image
Hakuna mpango wowote uliopo wa kufanyika video ya wimbo Hands Up ya Young Dee, kwa mujibu wa CEO wa Millian Dollar Boyz, Max Ryoba Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Max alisema badala yake itafanyika video ya wimbo mwingine kabisa. Amedai kuwa rapper huyo anaendelea kurekodi nyimbo huku pia msisitizo ukiwa katika kuangalia anaboresha afya yake kwa kula vizuri na kufanya mazoezi ya kutosha

Rufaa ya kutaka kuongezwa miaka ya kifungo cha Oscar Pistorius yakatwa upya

Image
Waendesha mashtaka wa Afrika Kusini, wamekataa rufaa mpya wakitaka kuwepo hukumu kali zaidi kwa Oscar Pistorius. Mwanariadha huyo mlemavu, alihukumiwa kifungo cha miaka sita kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake kwenye Valentine’s Day, 2013. Mwanzo kabisa alitumikia kifungo cha mwaka mmoja kati ya miaka mitano aliyokuwa amehukumiwa kwa kuua bila kukusudia, kabla ya hukumu kubadilishwa kuwa ya mauaji. Waendesha mashtaka wa South Africa’s National Prosecuting Authority (NPA) wanataka apewe kifungo kirefu zaidi. Reeva Steenkamp alikuwa na miaka 29 wakati anakufa.

Gavana BOT Afichua Siri ya Kilio Cha Fedha Kupotea Mtaani

Image
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo. “Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu. Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT. ...

Malawi Yadai Kuishtaki Tanzania Kwenye Umoja wa Afrika(AU)

Image
Foreign Affairs and International Cooperation minister Francis Katsaira said Tanzania has released a new Lake Malawi map which shows the east African country has taken a chunk of Lake Malawi, which is potentially rich in oil and gas.. “We have already reported them to the African Union and very soon we will be reporting them to Comesa and Sadc,” he said. Kasaira said Tanzanian authorities have threatened to beat up and arrest Malawians who will disregard the new map. The old map, drawn up by Germany and Britain gives the whole Lake Malawi, except a small part to Malawi. Tanzania has taken much interest in the lake after oil was discovered in the lake popularly known as lake of stars. Katsaira said both Malawi and Tanzania were supposed not to interfere with the Lake Malawi issue as the matter was with the African Union and a mediation team. He therefore said the government is waiting for a response from Tanzsnia on the proposal for Mutharika an...

Utafiti wa Twaweza: Watazania 96% wanampongeza Rais Magufuli

Image
Taasisi inayojishughulisha na kufanya tafiti mbalimbali nchini ya TWAWEZA. Leo imetoa ripoti inayoonyesha kuwa asilimia 96 ya Watanzania wapongeza utendaji wa Rais Magufuli, huku asilimia 68 wapongeza uwajibikaji wa wabunge wao. Aidha katika ripoti hiyo inabainisha kuwa jambo maarufu alilofanya Rais Magufuli ni uondoaji watumishi hewa huku zuio la kuingiza sukari likikosa umaarufu. Kiwango cha kukubalika cha Rais Magufuli katika utafiti mpya ni cha juu kuliko marais 128 wa Afrika

Wasanii na viongozi wa WCB waalikwa nyumbani kwa rais mtaafu Jakaya Kikwete

Image
Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana. JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye amesupport sana wasanii wa muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki wao. Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais huyo kwa kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu muziki. “Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam aliandika instagram

Congo DRC: Waasi wa Mai Mai wamewateka madereva 5 wa Tanzania, wanataka $ 4,000 kwa kila Dereva

Image
KUNA TAARIFA KUWA waasi wa Mai Mai wamewateka madereva wa Tanzania watano na kuchoma baadhi ya magari. Wanadai usd 4000 kwa kila Dereva amasivyo watawapiga risasi. Wametoa deadline ya majeshi kuondoka pia. Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka. TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics, Mzee Azim Dewji ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje tayari serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magariyaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ya Tanzania na 4 ya Kenya. M...

Namanga: Edward Lowassa asimamishwa na wananchi wamweleze ugumu wa maisha

Image
Mh Edward Lowassa Mjumbe wa kamati kuu wa chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) na Chama kikuu cha Upinzani TANZANIA na Waziri Mkuu mstaafu amesimamishwa na Wananchi wa Namanga Mpakani mwa Tanzania na Kenya .  Wananchi wamemueleza Ugumu na ukali wa Maisha walionayo ikiwa ni pamoja na kudorora kwa mzunguko wa fedha mpakani hapo leo hii akiwa safarini Toka Nairobi Kenya alipokwenda kuhudhuria mazishi ya Marehemu Ole Ntimama.