Mrema ayaomba makanisa kutenga sadaka za Jumapili moja kuwatoa wafungwa gerezani

Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa, Augustino Mrema ameyaomba makanisa nchini kutenga sadaka ya Jumapili moja kama harambee kwaajili ya kuwatoa baadhi ya wafungwa gerezan
Mrema ametoa pendekezo hilo, Alhamis hii.
“Ninachosema ifanyike harambee kwenye makanisa yote, tuangalie siku moja jumapili,wachungaji na maaskofu hizo sadaka msiwe mnazichukua tu ,chagueni Jumapili moja tu katika sadaka nyingi mnazokusanya, Jumapili moja sadaka zinazopatikana kwa siku hiyo zitumike kuwalipia faini wafungwa. Na baadhi ya waliofungwa ni wakristo wenu sio wapagani walioko magerezani, maana watu wanaweza wakachekelea wakifikiri sijui nini, ni wakristo waliobatizwa kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu, wakianguka kwenye dhambi wanapelekwa pale,” alisema.
“Ni kosa kwa mchungaji kuwa na mkristo yupo ndani kwa kushindwa kulipa faini ya shilingi elfu 50 anaendelea kusota, kwahiyo natoa wito hiyo sadaka isaidie kutoa wafungwa gerezani, ni pendekezo sio lazima wala sina uwezo wakuwaaamrisha,” amesisitiza.
Hivi karibuni, Mrema alimpongeza kiongozi wa kanisa la Mikocheni Assemblies of God, Askofu Getrude Rwakatare, alijitolea kuwatoa jela wafungwa 78 waliokosa fedha kulipia faini na hivyo kufungwa.
BY: EMMY MWAIPOPO

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU