MAREKANI YATOA RIPOTI YA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU


Wahamiaji nchini Libya
Wahamiaji nchini Libya
Kwa mara nyengine tena mwaka huu, sio tu taifa moja liloongoza ripoti hio, ambayo hutawaliwa na mataifa yaliyoendelea ya Magharibi kama vile Uingereza, Marekani na Australia.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inaeleza kuwa takwimu hizo zinalengwa zaidi juu ya kiwango cha hatua za serikali kukabiliana na biashara ya usafirishaji haramu kuliko kiwango cha tatizo la nchi.
Idadi kubwa ya mataifa ya kiafrika yanabaki katika chini ya orodha.
Susan Coppedge, mshauri mkuu kwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani anasema mzozo wa wahamiaji ambao umeona zaidi ya waafrika millioni moja, wairaqi na wasyria walotorokea ulaya mwaka jana umekuwa na athari mbaya. Anasema Marekani inajaribu kusaidia nchi wanazokimbilia kuweza kukagua waathiriwa wa biashara haramu ya usafirishaji .
Kwa hiyo mzozo wa wahamiaji umetengeneza kundi jipya la watu ambao ni dhaifu na wanaweza kutumiwa kwa biashara haramu ya binadam. Ikiwa hawana utaifa au hawana makaratasi rasmi , au hawana ajira au hawana familia, wanakuwa hatarini kwa kupewa ahadi za uwongo ambazo wafanya biashara haramu ya binadam wanawapatia kuwa watawapatia ajira, au usalama au makazi.
Jakob Christensen, mratibu wa mradi wa uwelewa dhidi ya biashara haramu ya binadam kundi linalopigana dhidi ya biashara hiyo huko Nairobi, anasema ana wasiwasi mkubwa kuhusu athari ya mzozo unaoendelea huko Afrika Mashariki na Afrika ya kati.
Nadhani tofauti kubwa ni kuwa mitindo ya uhamiaji ambayo tunayaona kwa wakati huu kutoka sehemu kama vile Burundi na Somalia na Afrika kusini.
Ripoti hiyo imetaja kuwa mwaka 2015, mataifa 6 barani Afrika yameboresha au kuanzisha sharia dhidi ya biashara haramu. Pia imetaja nchi ambazo zimeboresha hali hiyo, kama vile Burkina Faso ambayo ni nchi pekee iloonyesha kuboresha hali hiyo huko Afrika Magharibi, walizidisha juhudi zao za kuwashtaki na kuwafunga watu wanao fanya biashara haramu ya binadam.
Nchi 10 za kiafrika ziliweza kuingia katika orodha ya ripoti ya waizara ya mambo ya nje ya Marekani.
Hata hivyo ripoti hiyo inakiri kuwa hamna taifa ambalo halina matatizo, ikiwa ni pamoja na Marekani na kwamba kumaliza biashara haramu ya binadam ni jukumu kubwa na moja ambalo lina mizizi mingi. Hata hivyo ripoti inasema, tatizo hilo ni kubwa mno na haliwezi kudharauliwa.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU