Baba ajiweka tatoo kufanana na mwanawe aliyefanyiwa upasuaji.


Image captionBaba na mtoto

Baba wa miaka 28 nchini Marekani amenyoa kichwa chake na kuweka mchoro wa tatoo unaofanana na kovu la kichwa cha mwanawe aliyefanyiwa upasuaji.
Josh Marshall,ambaye anatoka Kansas aliingia katika shindano la kila mwaka linaloendeshwa na shirika la hisani kuhusu saratani ya watoto na kushinda taji la #BestbaldDad{baba mwenye kipara kizuri} wikendi iliopita.
Akikiri aliandika: Mimi na mwanangu katika hafla ya St. Baldtricks huko Wichita Kansas.
Niliwekwa tatoo ya kovu la mwanangu ili kuimarisha motisha yake.
Shindano hilo huwashirkisha watu wa familia na marafiki wa mtoto aliye na saratani.

Image captionBaba na mwanawe

Mwanawe alipatikana na uvimbe katika ubongo mnamo mwezi Machi.
''Mwanangu alikuwa na wasiwasi mwingi baada ya kufanyiwa upasuaji,alijihisi kama hayawani'',alisema Josh Marshal

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU