Nyimbo za R&B zinafanya vizuri zaidi kuliko nyimbo za hip hop.
Wasanii wa Hip Hop kaeni chonjo kwasababu takwimu za online zinaonesha kuwa nyimbo za R&B zinafanya vizuri zaidi kuliko nyimbo za hip hop.
Kwa mujibu wa Ismail Lossini kutoka mtandao wa Mkito, nyimbo za wasanii wa RnB akiwemo Ben Pol zinapakuliwa zaidi kwa sasa.
“Stats zimebadilika,” anasema. “RnB inaonekana kufanya vizuri zaidi ya hip hop,” Ismail alimweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Mtu kama Ben Pol amekuwa na releases nyingi sana na zimemweka kwenye sehemu nzuri kuweza kupandisha mahadhi ya RnB kuliko hip hop,” ameongeza.
Amedai kuwa wasanii wa hip hop wanaofanya vizuri ni Mr Blue na Young Killer.
“Kwa ujumla RnB inafanya vizuri kuliko hip hop kwenye chati za Mkito.”
Comments
Post a Comment