KOFFI AOMBA RADHI HADHARANI

Mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide ambaye mwezi July aliwasili  Nairobi Kenya  akiwa na wanamuziki wake pamoja na dancers wake kwa ajili ya show na baadae kuripotiwa kukamatwa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike ni baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akifanya kitendo hicho.

Koffi Olomide aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali,  na hiyo ilielezwa kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kulikuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.

Baada ya kupita miezi kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo na Koffi Olomide kutowahi kujitokeza hadharani kulizungumzia, amejitokeza kupitia kipindi cha Television cha Churchill Show amewaomba msamaha wakenya na mashabiki wake kwa ujumla na kusema …….

Kupitia Churchill show, nataka kusema na nyinyi na kutuma ujumbe wa upendo, heshima na urafiki, mimi nasikitika kwa kile kilichotokea na maombi yangu nisamehewe kwa kile kilichotokea, mimi ni mwanadamu tu licha kwa kuwa ni maarufu’:- Koffi Olomide

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU