Uislamu wapigwa marufuku Angola?
Ripoti za uongo kwamba Angola imekuwa taifa la kwanza duniani kupiga marufuku Uislamu zimezuka.
Clare Spencer anauliza iwapo hilo linahusishwa na uchaguzi wa urais nchini Marekani.''Waislamu wamekasirika sana'' ,aliandika Frank Lea katika gazeti la Freedom daily.
Angola kupiga marufuku Uislamu wanaodai ni madhehebu, na sio dini,ulielezea mtandao wa Libery Is Viral.
Habari hiyo inatoa maelezo kuhusu msikiti unaovunjwa katika eneo la Zango lililo jirani na mji mkuu wa Luanda.
Wanaona kile Waislamu wanavyowafanyia wale wasio Waislamu hususan barani Afrika,na wanachukua hatua kuzuia kutotokea hatua kama hiyo nchini Angola,habari iliochapishwa na mtandao wa ReaganCoalition.com.
Pengine huenda Marekani wakajifunza moja ama mawili kutoka kwa Angola,liliongezea gazeti la America First Patriots,ambalo linasema misikiti 80 imevunjwa.
Lakini habari hiyo sio ya kweli.Mtu mmoja mjini Luanda aliupiga picha msikiti huu mwezi uliopita ambao bado unafanya kazi.
Muislamu mmoja kutoka Angola Adam Campos,aliambia BBC kwamba jamii ya Kiislamu inaendelea kukuwa kila uchao.
Lakini Campos anasema msikiti wake ulifungwa na serikali miaka kadhaa iliopita,huku misikiti mingine ikiharibiwa wakat
Comments
Post a Comment