Rais MAGUFULI aongoza waombolezaji kumzika DIDAS MASABURI


Rais DKT. JOHN MAGUFULI ameongoza viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa na wakazi wa jijini DSM katika kuuaga mwili wa meya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkwe wake Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho katika mwili wa Marehemu Didas John Massaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Rais DKT. JOHN MAGUFULI ameongoza viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa na wakazi wa jijini la DSM katika kuuaga mwili wa meya wa zamani wa jijini la DSM, Dkt. DIDAS MASABURI.
Akizungumza katika viwanja vya KARIMJEE, Rais MAGUFULI amemwelezea Marehemu MASABURI kama mpiganaji mzuri wa Chama cha Mapinduzi.
Mwili wa marehemu MASABURI unazikwa jioni ya leo katika eneo la Chuo cha ununuzi na ugavi-IPS kilichoko CHANIKA katika wilaya ya ILALA.
Wakati wa uhai wake pamoja na mambo mengine Marehemu Dkt. MASABURI amewahi kushika nafasi mbalimbali kwenye Chama cha Mapinduzi-CCM,  na serikalini, hivyo familia imeona ni vyema watoe fursa ya kuagwa na wanasiasa wenzake pamoja na wakazi wa DSM.
Kabla ya kuwa meya wa jiji la DSM, Dkt. MASABURI amewahi kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU