Mlo wa viwavi wazua vita vya kikabila DRC

Viwavi ni mlo mtamu katika eneo la Katanga nchini DRC
Image captionViwavi ni mlo mtamu katika eneo la Katanga nchini DRC
Takriban watu 16 wameuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika vita vya kikabila huko mkoani Katanga ,kusini mashariki mwa taifa hilo kufuatia mgogoro wa kodi itakayotozwa viwavi.
Viwavi huwa ni chakula cha raia wengi wa taifa hilo wanaoishi Magharibi mwa taifa la DRC karibu na eneo lililo karibu na mji mkuu Kinshasa,ambao uko maili kadhaa kutoka Katanga eneo lililozuka vita.
Wadudu hao huchukuliwa kutoka kwa miti ,huchomwa na kuliwa na mchuzi.Viwavi hawawezi kusababisha vita katika taifa hilo hususan eneo la Katanga.
Mkoa huo hujulikana kwa kupenda kula viwavi hao na watu hawajauwana kwa sababu yao hapo mbeleni.
Lakini sasa kuna vita katika eneo hilo kati ya mbilikimo na makabila mengine.
Mbilikimo ndio wanaotoka katika eneo hilo lakini wanahisi wamebaguliwa kwa kukosa mali asili na elimu.
Kwa hivyo walipohisi kwamba chanzo kimoja cha mapato yao kinawekewa kodi,matokeo yakawa vita

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU