Mayanja akenua meno 32 Simba
NA SALMA MPELI,
KOCHA Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amechekelea kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuwaacha mbali watani wao wa jadi, Yanga.
Simba wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 23, wakifuatiwa na Stand United ambao wana pointi 20, huku Majimaji wakiendelea kuburuza mkia kwa pointi tatu.
Akizungumza na BINGWA jana, Mayanja alisema wanafurahi kuendelea kupata ushindi katika mechi zao, kwani inaonyesha jinsi gani walivyojipanga kuchukua ubingwa msimu huu.
“Tunashukuru kwa ushindi tunaoendelea kupata, lakini nitafurahi timu yetu kuendelea kuongoza ,” alisema Mayanja.
Mayanja alisema kwa sasa wataendelea kukinoa kikosi chao ili kiweze kutisha zaidi katika mechi zitakazofuata dhidi ya Mbao, itakayochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam
Comments
Post a Comment