Amini adai kuukubali zaidi wimbo wake ‘Robo Saa’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Amini Mwinyimkuu amedai kuukubali zaidi wimbo wake wa ‘Robo Saa’ kuliko nyimbo zake nyingine kwakuwa aliuandika kwenye mazingira magumu.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha 5 Selekt cha EATV kuwa wimbo huo aliuandika wakati alipokuwa mkoani Lindi na hakuwa na uwezo mkubwa zaidi.
“Wimbo huu nimeufanya kwenye mazingira magumu sana, nilikuwa siwezi kupiga guitar na niliuandika wakati nipo kijijini, Lindi nilipoenda kumtembelea mzee na hakukuwa hata na umeme,” amesema Amini.
Msanii huyo ameongeza kuwa kwa sasa hayupo THT tofauti na watu wengi wanavyodhania ila muda wowote akipigiwa simu anajumuika nao. Kwa sasa Amini anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Hawajui’ aliouachia mwezi Mei mwaka huu

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU