Mr Blue, Barakah Da’ Prince Wapatana

BAADA ya kutibuana kisa kikiwa Naj, hatimaye wakali wa Bongo Fleva, Mr Blue na Barakah Da’ Prince wameamua kuwa kitu kimoja.

Wawili hao walipatana saa chache kabla ya kufanyika Tamasha la Fiesta Shinyanga ambapo walikuwa wameenda kutembelea maporomoko ya Maji Moto pande za Shinyanga.

Tovuti hii ilipata nafasi ya kuchonga na Barakah akiwa pamoja na Mr Blue na kufunguka haya; “Ujue mambo yale
yalikuwa ya mpito tu, sasa hivi tumekuwa kitu kimoja kama unavyoona.”

Wawili hao waliingia katika bifu kali, baada ya Barakah kubamba namba ya simu ya Mr Blue katika simu ya Naj.

Fiesta inatarajia kukita nanga Tabora Ijumaa hii katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na Jumapili itakuwa ni zamu ya wakazi wa Singida kwenye Uwanja wa Namfua.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU