Maji ya mto yageuka 'rangi ya damu' Urusi

Norilsk, 8 Sep 16

Image copyrightAFP/GREENPEACE
Image captionMaji katika mto Daldykan yamekuwa ya rangi nyekundu
Wachunguzi wa masuala ya mazingira nchini Urusi wanajaribu kubaini chanzo cha maji ya mto ulio karibu na kiwanda cha nikeli cha kampuni ya Norilsk Nickel yamebadilika rangi na kwua na rangi nyekundu.
Picha za maji ya mto Daldykan ambayo yamebadilika rangi zimesambazwa sana katika vyombo vya habari Urusi.
Gazeti la serikali la Rossiiskaya Gazeta linasema kuvuja kwa bomba la kusafirisha taka za mchanganyiko wa shaba nyekundu na nikeli huenda likawa kiini cha maji hayo kubadilika rangi.
Norilsk Nickel ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa nikeli na palladium duniani.
Zvezda TVImage copyrightSCREENSHOT
Image captionPicha za runinga ya wizara ya ulinzi ya Zvezda TV
Kampuni hiyo ina vinu na tanuri nyingi rasi ya Taimyr eneo la Krasnoyarsk katika jimbo la Siberia. Ujenzi wa vinu hivyo vikubwa ulifanyika enzi za muungano wa Usovieti.
Kampuni hiyo ina kiwanda kwa jina Nadezhda karibu na mto Daldykan lakini maafisa wake wanasema hawajapata dalili zozote za uchafuzi kutoka kwa kiwanda hicho.
Rais wa kampuni hiyo ni bilionea Vladimir Potanin.
Russia Norilsk map

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU