Mwanamke avunja rekodi ya ndevu ya Guinness World Record
Mwanamitindo mwenye ndevu za urefu wa inchi sita ametambuliwa na Guinness World Record kuwa mwanamke wa umri mdogo zaidi duniani kuwa ndevu zilizokomaa kabisa.
Harnaam Kaur, 24, ambaye ni mwanamke mtetezi wa kutambuliwa na kukubalika kwa hali ya mwili wa mwanadamu ulivyo bila ubaguzi anatoka Slough, Berkshire nchini Uingereza.
Amesema ni heshima kubwa kwake kutambuliwa.
Ameeleza ndevu hizo ndefu kama sehemu ya juhudi zake za kukabiliana na watu wengi waliomkejeli kutokana na muonekano wake.
Wengine waliotambuliwa kwenye rekodi za karibuni zaidi ni paka mrefu zaidi anayefugwa kama mnyama kipenzi pamoja na Ilama anayeruka juu zaidi.
Bi Kaur ana tatizo la homoni lifahamikalo kwa Kiingereza kama polycystic ovary syndrome, ambalo humfanya mwanamke kuwa na nywele zaidi kuliko kawaida usoni.
Machi 2016 Harnaam Kaur alikuwa mwanamke wa kwanza kushiriki maonyesho ya mitindo ya London Fashion Week akiwa na ndevu.
'Rekodi ya llama'
Rekodi ya paka mrefu wa kufugwa nyumbani ambaye bado yuko hai imemwendea paka kwa jina Ludo kutoka Wakefield, West Yorkshire ambaye urefu wake ni 3ft 10.59in (1.183m).
Caspa, wa miaka tisa, naye ametambuliwa kwa kuruka juu. Anaweza kuruka juu 3ft 8.5in (1.13m).
Anaishi Porthmadog, Wales Kaskazini.
Comments
Post a Comment