Trump asisitiza kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji
Mgombea urais wa chama cha Rupublican nchini Marekani Donald Trump amesema kuwa atabuni mfumo ambao utasaidia serikali kudhibiti uhamiaji.
Akizungumza wakati wa kampeni katika jimbo la Iowa bwana Trump alisema kuwa mfumo huo utasaidia kuwatimua watu ambao wanaishi nchini Marekani licha ya muda wa visa zao kumalizika.
Pia alirejelea wito wake wa kujengwa ukuta kati ya mpaka wake na Mexico kuwazuia wahamiaji
Comments
Post a Comment