Vijana 6 kula shavu kwa Kala Jeremiah
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amewataka vijana 6 kuchangamkia fursa ya kushiriki katika remix yake ya wimbo ‘WanaNdoto’.
Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘WanaNdoto’ amewataka vijana kumtumia clips za video wakiimba mashairi ya kuwatia moyo watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu.
“Tunatafuta watu 6 watakaofanya remix ya ‘WanaNdoto’ kama unajua unauwezo andika mistari yako inayoongelea watoto yatima na wale wote waishio kwenye mazingira magumu kisha jirecord ukiimba mistari hiyo kisha post kwenye ukurasa wako wa instagram kisha hustag neno ‘WanaNdoto’ tutaiona tutaipost hapa kisha watu sita ambao video zao zitapata likes nyingi watachaguliwa kushiriki kwenye remix official ya ‘WanaNdoto’siyo lazima uimbe juu ya beat kama huyu hata ukiimba kavu kavu utaeleweka tu,” alitoa taarifa Kala kupitia instagram yake.
Video ya wimbo ‘WanaNdoto’ inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya runinga kutokana na muimbaji huyo kuimba vitu ambavyo vinawagusa wananchi wa chini
Comments
Post a Comment