Rais MAGUFULI aagiza Raia kuondolewa ndani ya Jeshi


Rais Dkt JOHN MAGUFULI amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini-IGP ERNEST MANGU kuwaondoa Raia walioajiriwa ndani ya Jeshi la Polisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi DCP na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Dkt JOHN MAGUFULI amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini-IGP ERNEST MANGU kuwaondoa raia walioajiriwa ndani ya  Jeshi la Polisi na kuwapeleka utumishi ili wapangiwe majukumu mengine.
Rais MAGUFULI amesema hayo jijini DSM, wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Naibu Makamishna 25 na Makamishna wasaidizi 35 waliopandishwa vyeo wiki iliyopita, ambapo ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kujiangalia upya pale ambapo linatoa nafasi mbalimbali za ajira kwa raia badala ya maafisa wa polisi.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini-IGP, ERNEST MANGU ametoa wito kwa maafisa hao kutenda majukumu hayo kwa mujibu wa sheria na kwamba hatasita kuchukua hatua kwa maafisa watakaokiuka viapo vyao vya kazi.

Zoezi la kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma limeendeshwa na Kamishna wa Maadili kwa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu SALOME KAGANDA, ambaye amesema jeshi la polisi ni kiungo muhimu kwa usalama wa taifa

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU